Katibu
wa kamati ya serikali ya maandalizi ya mbio za Uhuru marathon Tanzania
Innocent Melleck Katikati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar
Es Salaam juu ya udhamini wa kampuni ya bia nchini Tbl kupitia kinywaji
chake kisicho na kilevi cha GrandMalt ambapo kimetoa jumla ya shilingi
milioni ishirini (20,000,000) kushoto ni mkurugenzi msaidizi wa idara ya
habari maelezo Tiganya Vincent na kulia ni meneja masoko wa Tbl Fimbo
Butalla
Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI
ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake kisicho na kilevi cha
GrandMalt imejitokeza kudhamini mbio ndefu za Uhuru, Uhuru Marathon, kwa
kiasi cha Sh milioni 20.
Akitangaza
udhamini huo jijini Dar es Salaam jana, Meneja Masoko wa TBL, Fimbo
Butallah alisema, wameona ni vyema kudhamini mbio hizo kwani zina lengo
zuri zaidi la kuimarisha umoja, amani na mshikamano miongoni mwa
Watanzania.
Kuhusu
udhamini huo, Butallah alisema, Sh milioni 13.4 zitatumika kwa ajili ya
kutoa zawadi mbalimbali kwa washindi, huku Sh milioni 6.6 zikiwa ni kwa
burudani zitakazofanyika siku ya mkesha wa kuamkia mbio hizo.
“Ukweli
ni kwamba taifa lolote duniani linapigania kuwa na uchumi imara na
pasipokuwa na amani hakuna uchumi utakaoweza kukua, hivyo TBL kama
kampuni inayotengeza bidhaa za hapa nyumbani imeona ni muhimu kuungana
na Watanzania wenzetu wote kuhakikisha kuwa mbio hizi zinafanyika katika
hali ya mafanikio makubwa na kuwa za kufana zaidi.
“Nitoe
rai pia kwa makampuni ya ndani na nje ya nchi kujitokeza na pia
kuendelea kutoa chochote walichonacho ili kufanikisha mbio hizi zenye
kubeba dhima ya Taifa letu lakini pia wajitokeze kwa wingi kushiriki
mbio hizi.
“Kwa
zawadi hizi tulizotangaza leo tunaamini zitakuwa kichocheo kwa
wakimbiaji wetu kufanya mazoezi ya kutosha ili kuhakikisha fedha hizi
zinabaki ndani ya ardhi ya Tanzania,” alisema.
Naye
Katibu wa Kamati ya Uhuru Marathon, Innocent Melleck aliwaomba
Watanzania kujitokeza kwa wingi kushiriki mbio hizo ambazo zina nia
kubwa ya kutukumbukusha wajibu wetu wa kutunza na kulinda amani, umoja
na mshikamano miongoni mwetu.
Alisema
zawadi kwa mshindi wa kwanza inatarajiwa kuwa Sh 1,500,000 kwa
wakimbiaji wa kilomita 21 na 42, hii ni kwa upande wa wanawake na
wanaume.
Mshindi
wa pili kwa mbio hizo iwe kwa upande wa wanawake au wanaume kwa
kilomita 21 au 42 ataondoka na Sh 800,000 wa tatu Sh 600,000 wanne Sh
300,000 na watano apata Sh 150,000.
Mbio
hizi zinatarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam hapo Desemba 8, mwaka
huu ambapo zitaanzia na kumalizikia katika Viwanja vya Leaders club.
Rais
Jakaya Kikwete anatarajiwa kushiriki mbio hizi, huku wabunge zaidi ya
100 wakiongozwa na Spika Anne Makinda wakiwa wamejisajili kwa ajili ya
kushiriki.
Mbio
hizo zimegawanywa katika makundi makuu manne ambayo ni kilomita 3 kwa
ajili ya viongozi, kilomita 5 kwa watu wote na kilomita 21 na 42 ambazo
ni maalum kwa wakimbiaji nguli.
0 comments:
Post a Comment