Safari ya fundi fataki kwenda jela mwaka mmoja ikianzia hapa
………………………………………………………….
Na Francis Godwin Blog
FUNDI
magari mkazi wa kijiweni katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa
Bw Abdul Husein (31) amejikuta akitupwa jela mwaka mmoja na faini
ya shilingi 200,000 baada kutiwa hatiani na mahakama ya mwanzo
bomani kwa kosa la kutaka penzi la nguvu kwa mwanafunzi wa darasa
la tano .
Fundi
huyo ambaye anadaiwa kukaribishwa katika nyumba hiyo kama mlinzi
wa watoto wawili akiwemo mwanafunzi huyo wa miaka 11 alitenda kosa
hilotarehe 4 mwezi huu majira ya saa 3 usiku baada ya kurejea
kutoka katika shughuli zake.
Akisoma
hukumu hiyo leo hakimu mkazi wa mahakama ya mwanzo bomani
mheshimiwa Alois Masua alisema kuwa katika ushahidi ambao
ulitolewa mahakamani hapo na mtoto wa kiume wa miaka 9 ulidai kuwa
kijana huyo siku ya tukio baada ya kufika nyumbani alimtaka binti
huyo kumpa sahani ili aweke chips ambazo alikuja nazo .
Kuwa
baada ya binti huyo jina limehifadhiwa na mtandao huu kumpa sahani
ndani ya dakika chache aliomba kupewa maji na binti huyo alifanya
hivyo baada ya kupewa maji kijana huyo alimtaka binti huyo kusogea
kukaa katika eneo kochi ambalo fundi huyo amekuwa akilitumia kama
kitanda chake sebuleni kama mlizi bado binti huyo aligoma kuingia
majaribuni .
Hata
hivyo haikuishia hapo baada ya muda fundi huyo fataki alimtaka
binti huyo kumsindikiza chooni bado binti alionyesha msimamo wa
kutamani masomo yake na kugoma kumsindikiza kwa madai kuwa yeye ni
binti na huyo ni mwanaume iweje aombe kusindikizwa .
Kutokana
na mbinu zote kugonga mwamba ndipo fundi fataki huyo alipoamua
kutumia njia ya mkato ya kumkamata kwa nguvu binti huyo na kutaka
kumbaka chooni kabla ya binti huyo kuamua kupambana na kuishia
kuchaniwa sketi yake .
Hali
hiyo ilimfanya binti huyo kutimua mbio na kuomba msaada kwa mama
yake aliyekuwa amelala chumba cha pili kabla ya mama mzazi na
majirani kuamka na kumwadabisha fundi fataki kwa kumpeleka polisi.
Hakimu
Masua alisema kuwa kutokana na ushahidi uliotolewa fundi huyo
alipotakiwa kujitetea alikana kujitetea kwa madai kuwa hawezi
kuzungumza chochote katika mahakama hiyo.
Hivyo
alisema kutokana na mtuhumiwa huyo kutenda kosa hilo kwa mara ya
kwanza mahakama hiyo ilipaswa kumfunga jela kwa miaka mitano
kutokana na kosa hilo la shambulio la aibu kifungu cha 135 kanuni ya
adhabu namba 6 marejeo mwaka 2002 .
“
Mahakama hii inakuona na hatia na hivyo inakupunguzia adhabu
kutoka miaka mitano uliopaswa kutumikia na kufungwa mwaka mmoja jela
na ukitoka utatakiwa kumlipa mlalamikaji kiasi cha Tsh 200,000”
|
0 comments:
Post a Comment