Waziri wa wizara ya mambo ya ndani ya nchi, Dkt. Emmanuel Nchimbi
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kutokana
na Maboresho yanayoendelea ndani ya Jeshi la Polisi kumekuwepo na
mikakati mbalimbali inayolenga uboreshaji wa miundombinu yake, ikiwa ni
pamoja na kupata ofisi, vituo vya polisi, makazi ya kuishi askari
makambini, vifaa na vitendea kazi ili kuimarisha ulinzi na usalama
nchini.Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kupitia Jeshi la Polisi iliona
kuna umuhimu wa kuanzisha Shirika la uzalishaji mali la Polisi
(Tanzania Police Corporation Sole) ili kuendelea kufanikisha malengo ya
maboresho yanayoendelea.
Kufuatia
hatua hiyo Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
aliridhia kuanzishwa kwa Shirika la Uzalishaji ndani ya Jeshi la Polisi
baada ya kusaini Amri ya uanzishwaji Shirika hilo tarehe 27/9/2012 kwa
mujibu wa sheria ya mwaka 1974 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2000.
Mara
baada ya kusainiwa na Mheshimiwa Rais, Mheshimiwa Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, kwa mujibu wa sheria ameteua Bodi ya Shirika hili na
kumteua Ndugu EMMANUEL HUMBA kuwa Mwenyekiti wa Bodi hiyo kwa miaka
mitatu kuanzia tarehe 19/9/2013, aidha amewateua wajumbe wafuatao kuwa
wajumbe wa Bodi hiyo:-
(1)Mwakibinga E.P.M Mihalale- Msajili wa Hazina Msaidizi
(2)Jehad Abdallah Jehad –Msajili Bodi ya Wakadiriaji na Wasanifu
Majengo
(3) Melkior Temu- Mipango, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
(4) T.M.E Andengenye –DCP Mkuu wa Utawala Jeshini
(5) A. Nyamhanga –ACP-Mkuu wa Kitengo cha Mipango na Bajeti Jeshi la
Polisi
(6)Samwel Marco-Meneja Hazina –(Tressure)-TIB
(7) John Mathew- Kaimu Mkurugenzi Mhamasishaji- TIC
Katika
uteuzi huo amemteua pia DCP- SOSPETER M. KONDELA kuwa Mkurugenzi
Mtendaji wa Kwanza wa Shirika hilo .uteuzi huo unaanza mara moja.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI,
18 NOVEMBA, 2013.
0 comments:
Post a Comment