GWIJI wa muziki wa dansi, Muhidin Maalim Gurumo ameugua ghafla mapema leo na kulazwa Hospitali yaTaifaMuhimbili.
Wajumbe
wa Kamati ya maandalizi yaTamasha la Gurumo, Juma Mbizona Said Mdoe,
waliokuwepoMuhimbili, wameuambia mtandao huu kuwa mwimbaji huyo mkongwe
alipatwa na tatizo la shinikizo la damu na hali ikawa mbaya kabla ya
kukimbizwa hospitalini hapo.
Wamesema kwasasa hali yake inaendelea vizuri na amelazwa katika wodi ya Mwaise la namba 1.
Wajumbe
hao wamesema siku chache zilizopita, Gurumo alikuwa kwenye afya njema
na hata siku ya Jumanne alihudhuria kikao cha kamati hiyo kilichofanyika
Vijana Social Hall Kinondoni.
Aidha,
wajumbe hao wamedai kuwa kwamujibu wa mke wa Gurumo, Bi Pili, ni kwamba
hata jana mwimbaji huyo alikuwa hana tatizololote na alifanya mizunguko
yake bila ya mikwaruzo yoyote.
Mwenyekiti
wa kamati ya maandalizi ya tamasha la Gurumo, Bi Asha Baraka amewataka
wapenzi wa muziki kuwa watulivu kwa vile hali ya mwanamuziki huyo
aliyeitumikia fani kwamiaka 53, inaendeleavizuri.
Tamasha la Gurumo limepangwa kufanyikat arehe 14 mwezi ujao katikav iwanja vya TCC Club Chang’ombe.
Tumuombee dua mzee wetu Gurumo.
0 comments:
Post a Comment