Makamu
wa Rais wa Taasisi ya Uongozi ya Jamhuri ya Watu wa China Mh.Hong Yi
akimkabidhi nakala ya kitabu chenye nasaha za watu mashuhuri kutoka
jamhuri ya watu wa China Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue ikulu
jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mkuu wa Taasisi ya Uongozi
Tanzania Profesa Joseph Semboja. Awali viongozi hao wawili walifanya
mazungumzo yenye lengo la kuimarisha uhusiano kati ya Taasisi ya Uongozi
ya China na ile ya Tanzania.Taassisi hizo mbili zinatarajia kutia saini
mkataba wa ushirikiano wiki hii.
Taasisi
ya Uongozi Tanzania(Uongozi Institute pamoja na Taasisi ya Uongozi ya
China(Chinese Academy of Governance) zinatarajiwa kusaini Mkataba
wakukuza ushirikiano kati ya taasisi hizo mbili Jumanne wiki ijayo
jijini Dar es Salaam.
Mkuu
wa Taasisi ya Uongozi Institute Profesa Joseph Semboja ameyasema hayo
jijini Dar es Salaam leo baada ya Ujumbe kutoka Taasisi ya Uongozi wa
China( Chinese Academy of governance) kumtembelea Katibu Mkuu Kiongozi
Balozi Ombeni Sefue ikulu jijini Dar es Salaam.
Ujumbe
huo kutoka Jamhuri ya Watu wa China unaongozwa na makamu wa Rais wa
Taasisi hiyo Bwana Hong Yi na ziara hiyo inafuatilia ziara ya hivi
karibuni ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda ambayo pamoja na mambo mengine
uhusino kati ya taasisi hizo mbili ulitiliwa mkazo.
Profesa
Semboja aliongeza kusema kuwa mkataba wa mahusiano kati ya taasis hizo
utawezesha ubadilishanaji wa teknolojia na utaalamu na hivyo kuboresha
mafunzo yanayotolew na taasisi ya Uongozi Tanzania.
Kwa
upande wake Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue alimshukuru Bwana
Hong Yi kwa nia yake njema ya kushirikiana na Taasisi ya Uongozi
Tanzania na kuongeza kuwa ushirikiano kati ya China na Tanzania ni
wakihistoria na wenye manufaa makubwa kwa wananchi wa nchi hizo mbili.
Katibu
Mkuu balozi Ombeni Sefue akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais
wa Taasisi ya Uongozi ya China Mh.Hong Yi ikulu jijini Dar es Salaam
leo(picha na Freddy Maro)
0 comments:
Post a Comment