Tuesday, November 19, 2013

Magessa-Mulongo 
Na Gladness  Mushi, Arusha
Katika hali isiyokuwa ya kawaida mkuu wa mkoa wa Arusha Magesa Mulongo ametangaza utaratibu mpya kwa wakurugenzi ambapo kuanzia sasa wataomba ruhusa za kwenda nje ya wilaya au mkoa kwa sababu maalumu
Aidha utaratibu huo unakuja mara baada ya mkuu huyo kudai kuwa wakurugenzi wote wa jiji la arusha wanaweza kuongeza ufanisi wa maendeleo lakini pia wakapunguza kasi ya maendeleo
Mulongo aliyasema hayo mapema wiki hii wakati akiongea na viongozi wa vijiji kutoka maeneo mbalimbali jijini hapa huku lengo halisi la kukutana nao likiwa ni kujadili namna ya kuongeza mafanikio ya miradi iliopo kwenye ngazi za vijiji
Mulongo alisema kuwa kwa wakurugenzi wote wa Jiji la Arusha kuanzia sasa wataomba ruhusa maalumu kwa wakuu wa wilaya lakini pia kwenye ofisi yake ili kupunguza tatizo la kutoka nje ya ofisi kila mara
Aidha alidai kuwa utaratibu huo wa kuomba ruhusa utaweza kupunguza kasi ya safari ambazo hazina tija kwenye Halmashauri hivyo basin itaweza kuruhusu maendeleo kwa wananchi kwa haraka sana tofauti na sasa ambapo wakitaka kwenda mahala popote pale wanakwenda.
Wakati huo huo pia alisema kuwa mbali na kuomba ruhusa kwa wakuu wa wilaya lakini pia hata katika ofisi yake ni lazima pia watambue wana nafasi kubwa sana ya kuwasaidia wananchi na wala sio kukaa maofisini kama wanavyofanya baadhi yao kwa sasa
Alisema kuwa wakurugenzi kwa kushirikiana na wakuu wa idara sasa wanapaswa kutembea kwa wananchi zaidi kuliko kuipenda ofisi na endapo kama watakiuka agizo hilo ambalo linaenda katika wilaya zote za Jiji la Arusha basi watachukuliwa sheria kali
Pia aliwataka viongozi kuanzia ngazi ya Kitongoji kuhakikisha kuwa wanaweka utaratibu wa kutambua miradi iliopo kwenye kata ili kuweza kuwabana baadhi ya viongozi wa Serikali ambao wanatumia miradi hiyo kwa ajili ya kujinufaisha.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video