Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwapungia wananchi wa kijiji cha Nyumbigwa wilayani Kasulu kabla ya kuweka jiwe la msingi la mradi wa maji wa kijiji hicho akiwa katika ziara ya mkoa wa Kigoma, Oktoba 4, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na mmoja wa watoto waliohudhuria katika mkutano wa hadhara aliouhutubia katika kijiji cha Nyumbigwa wilayani Kasulu akiwa katika ziara ya mkoa wa Kigoma Oktoba 4, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiweka jiwe la Msingi la Mradi wa Maji wa Kijiji cha Nyumbigwa wilayani Kasulu akiwa katika ziara ya mkoa wa Kigoma Oktoba 4, 2013. Kushoto ni Naibu Waziri wa Maji, Dkt Benilith Mahenge(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)Mabango ambayo yaliyoonyeshwa na wanachi wa kijiji cha Nyumbigwa wilayani Kasulu katika mkutano uliohutubiwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kijijini hapo akiwa katika ziara ya mkoa wa Kigoma, Septemba 4, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwaagiza wakuu wote wa Idara katika katika wilaya mpya ya Buhigwe (pichani) kuhamia kwenye makao makuu ya wilaya hiyo ifikapo mwisho wa mwezi wa Desemba ili washughulikie matatizo ya wananchi na kuleta maendeleo. Hivi sasa watumishi hao wanaishi mjini Kasulu, Mheshimiwa Pinda yuko katika ziara ya mkoa wa Kigoma Oktoba 4, 2013, (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akipokea zawadi ya kinyago cha kuku jike na dume wakiwa na vifaranga kutoka kwa Mkuu wa Makazi katika Kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu iliyopo wilayani Kasulu , Fredrick Nisajile katika mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda katika kijiji cha Nyumbigwa Oktoba 4, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Wanakwaya wa Buhigwe wakiimba wakati Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alipozindua wilaya hiyo akiwa katika ziara ya mkoa wa Kigoma Oktoba 4, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)Wasanii kutoka wilaya ya Mabanda nchini Burundi wakicheza ngoma ya Mtiimbo katika sherehe za uzinduzi wa wilaya mpya ya Buhigwe uliofanywa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa katika ziara ya mkoa wa Kigoma Oktoba 4, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
0 comments:
Post a Comment