Hakimu
Mahakama ya Mwanzo ya Kerege iliyopo Wilayani Bagamoyo Judas Kyombo
akisoma taarifa fupi ya utendaji ya mahakama hiyo alipotembelewa Naibu
Waziri wa Katiba na Sheria Angellah Kairuki alipokuwa kwenye ziara ya
siku moja wilayani humo.

Picha ya pamoja ya Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Angellah na
watumishi wa Mahakama ya Mwanzo ya Kerege iliyopo Wilayani Bagamoyo mkoa
wa Pwani alipokuwa kwenye ziara ya siku moja wilayani humo.

Naibu
Waziri wa Katiba na Sheria Angellah akisisitiza umuhimu wa kutoa adhabu
mbadala kwa watuhumiwa baada ya hukumu zao kukamilika alipokuwa
anaongea na watumishi wa Mahakama ya Mwanzo ya Kerege (hawapo pichani)
iliyopo Wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani kwenye ziara yake ya siku moja
wilayani humo. Wa kwanza kushoto ni Hakimu Mkazi Mfawidhi Mkoa wa
PwaniBahati Ndeserua, wa kwanza kushoto ni Msajili Mahakama kuu, kanda
ya Dar es salaam Projestus Mhagama.

Hakimu
Mfawidhi Mahakama ya Wilaya ya Bagamoyo Liadi Mohamed Chamshama
akimwonesha Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Angellah (mwenye gauni
kitenge) na ujumbe wake eneo la mahakama ya Mwanzo ya Kiwangwa alipokuwa
kwenye ziara ya kikazi ya siku moja wilayani mkoa wa Pwani.
0 comments:
Post a Comment