
Katika mazoezi ya jana Jumatano asubuhi, wachezaji wote waliamkia
ufukweni kujiweka fiti kama Simba wanavyofanya kwenye Ufukwe wa
Kigamboni.
BAADA
ya kuifunga Chipukizi ya Pemba mabao 2-1 jana Jumatano, Kocha wa Yanga,
Ernest Brandts, amewatuliza mashabiki wa timu hiyo akiwaambia kwamba
mambo yanakwenda sawa hivyo wasiwe na mchecheto kuhusiana na mechi dhidi
ya Simba.
Kuthibitisha hilo jana Jumatamo
aliwakimbiza wachezaji wake kwenye mchanga wa ufukweni kwa saa tatu
mfululizo huko Pemba, ambako wameweka kambi kabla ya jioni yake kuifunga
mabao 2-1 timu ya Chipukizi katika mchezo wa kirafiki uliofanyika
kwenye Uwanja wa Gombani.
Bao la kwanza katika mchezo huo
lilifungwa na Jerry Tegete kabla ya Abdallah Mguhi ‘Messi’ kufunga la
pili katika mechi ambayo Yanga ilitumia wachezaji wengi wa kikosi cha
pili.
Yanga imewekwa chini ya ulinzi
wa meneja maalumu wa kambi, Maneno Hussein, ambaye kazi yake ni
kuhakikisha hakuna yeyote asiyehusika anayejipenyeza kuingia kambini
hapo kwenye hoteli ya Samail mjini Pemba ili kuzungumza na wachezaji.
Katika mazoezi ya jana Jumatano
asubuhi, wachezaji wote waliamkia ufukweni kujiweka fiti kama Simba
wanavyofanya kwenye Ufukwe wa Kigamboni.
Yanga ambayo imekuwa ikibadili
programu zake za mazoezi kuhakikisha inakuwa fiti kwa mechi hiyo ya
Jumapili, jana jioni ilicheza na Chipukizi kwenye Uwanja wa Gombani,
lakini ikatumia kikosi cha pili na kuibuka na ushindi wa 2-1..
Kikosi kilichoanza ni Deo
Munishi, Juma Abdul, Oscar Joshua, Ibrahim Job, Rajab Zahor, Hamis
Thabit, Simon Msuva, Nizar Khalfan, Jerry Tegete, Husein Javu na Said
Bahanuzi.
Yanga iliwasili Pemba Jumatatu,
mara tu ilipotua iliingia moja kwa moja uwanjani kufanya mazoezi mchana
wa jua kali. Lakini siku iliyofuata yaani juzi Jumanne, ikaingia kupiga
tizi kwenye Uwanja wa Gombani kwa saa mbili kuanzia saa tatu asubuhi.
Jana Jumatano ikafanya mazoezi ufukweni kuanzia saa 3 asubuhi mpaka saa 5 asubuhi.
“Hatuwezi kuidharau Simba, kwani
ni moja ya timu nzuri na ndio maana inaongoza ligi, hivyo naamini
wamejipanga na wamejiandaa na hata sisi tunajiandaa kwa sehemu yetu,
lengo ni kuhakikisha tunapata pointi tatu katika mchezo huo,” alisema
Brandts.
“Tutaikabili Simba kama timu
nyingine kwenye ligi, najua utakuwa mchezo wa upinzani sana kwa sababu
tunakutana timu kubwa mbili pinzani hapa nchini, lakini tusubiri dakika
90. Ila ninawaahidi mashabiki wetu watafurahia soka kutoka kwetu.
“Nimewaona
Simba katika baadhi ya mechi, najua wanavyocheza kwa kila mchezaji wao,
najua udhaifu wao na mbinu zao ingawa siwezi kuzitaja kwani zitabaki
katika makabrasha yangu, ila nitatumia udhaifu wao kuwamaliza.
“Ninachofurahi sina majeruhi, Ngassa (Mrisho) anaumwa malaria lakini
anafanya mazoezi mepesi, kadiri muda unavyokwenda afya yake inazidi
kuimarika, pia Telela (Salum) naye anaendelea vizuri, ninachoomba mpaka
kufika siku hiyo wachezaji wote wawe fiti kwa asilimia 100.”
CHANZO: MWANASPOTI
0 comments:
Post a Comment