Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail
KOCHA wa Washika bunduki wa kaskazini mwa London, klabu ya Asernal, Mfaransa, Arsene Wenger amesifu kuwasili kwa Mjerumani Mesut Ozil na kusema kuwa kumuongezea imani kubwa baada ya kumtazama nyota huyo katika mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Napoli jana usiku ambapo Gunners walishinda mabao 2-0 Emirates.
Katika mchezo wa jana, Ozil alimalizia krosi ya Aaron Ramsey na kuandika bao la kuongoza na alitoa pasi ya bao la pili la Olivier Giroud .
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 24 na aliyeongoza kushangilia na Giroud baada ya kipenga cha mwisho, alijiunga na Arsenal akitokea Real Madrid kwa ada ya uhamisho ya pauni milioni 43 majira ya kiangazi mwaka huu na Wenger amejisifu kwa mafanikio hayo.




0 comments:
Post a Comment