Kamishna
Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja (wa kwanza kushoto)
akimkaribisha Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Dkt. Emmanuel
Nchimbi tayari kwa ufunguzi wa Mkutano wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la
Magereza leo Oktoba 23, 2013 katika Ukumbi wa Hoteli ya Edema, Mkoani
Morogoro, wa pili kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya
nchi, Mhe. Mbarak Abdulwakil(wa tatu kushoto) ni Mkurugenzi wa Sera na
Mipango Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Haji Janabi(wa nne kushoto) ni
Kamishna wa Huduma za Urekebishaji, Deonice Chamulesile(wa pili kulia)
ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa na wa
kwanza kulia ni Kamishna wa Fedha na Utawala, Gaston Sanga.
Kamishna
Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja akitoa maelezo mafupi ya
utangulizi kabla ya kumkaribisha rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhe. Dkt. Emmanuel Nchimbi(hayupo pichani) kufungua rasmi Mkutano
wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza ambao unafanyika katika
Ukumbi wa Hoteli ya Edema, Mkoani Morogoro.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Dkt. Emmanuel Nchimbi akitoa hotuba ya
ufunguzi kwa wajumbe wa Mkutano wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la
Magereza( hawapo pichani) katika Ukumbi wa Hoteli ya Edema, Mkoani
Morogoro.
Baadhi
ya Wajumbe Washiriki katika Mkutano wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la
Magereza wakisikiliza hotuba ya Mgeni rasmi(hayupo pichani) wakati wa
ufunguzi wa Mkutano wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza katika
Ukumbi wa Hoteli ya Edema, Mkoani Morogoro.
Waziri
wa Mambo ya ndani ya Nchi, Mhe. Dkt. Emmanuel Nchimbi( wa nne kushoto)
akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza
kwa waliosimama katika picha mara baada ya kufungua rasmi Mkutano huo
leo Oktoba 23, 2013 wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza
utakaofanyika kwa siku mbili katika Ukumbi wa Hoteli ya Edema, Mkoani
Morogoro( kushoto kwa Waziri) ni Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhe. Mbarak Abdulwakil( kulia kwa Waziri) ni Kamishna Jenerali wa
Magereza, John Casmir Minja. Wengine ni Mkurugenzi wa Sera na Mipango
wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Haji Janabi(wa kwanza kushoto), wa
pili kushoto ni Kamishna wa Huduma za Urekebishaji, Deonice
Chamulesile(wa tatu kulia) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa
Magereza, Dkt. Juma Malewa na wa pili kulia ni Kamishna wa Fedha na
Utawala, Gaston Sanga. Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza.
0 comments:
Post a Comment