Wednesday, October 16, 2013

DSC_4925 
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
HATIMAYE Ashanti United `Watoto wa jiji` waanza kuonja ladha ya ushindi katika mikikimikiki ya ligi kuu soka Tanzania bara baada ya jioni ya leo kuibuka na pointi tatu nyingine muhimu mbele ya Tanzania Prisons `Wajelajela` kutokana na ushindi wa mabao 2-1 uwanja wa Azam Complex, Chamaz, nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.
Bao la ushindi limetiwa kimiani dakika za lala salama, lala kwa buriani ambazo hazimruhusu hata kuku kumeza punje ya mchele na Mwinyi Ally.
Ally  aliyetokea benchi dakika ya 83 kuchukua nafasi ya Fakhi Hakika, alipachika bao hilo lililoleta raha kubwa kwa mashabiki wa Ashanti ambao walishaanza kuvunjika moyo baada ya kutokea pukurushani katika lango la maafande hao wa Magereza wenye makazi yao jiji Mbeya.
Hadi mapumziko, timu hizo zilikuwa zimechoshana nguvu kwa kuburuzana bao 1-1 ambapo Prisons walitangulia kupata bao dakika ya nne kupitia kwa John Matei na beki Tumba Sued akaisawazishia Ashanti dakika ya 21.
Kiujumla Prisons inayofundishwa na kocha mkuu Jumanne akisaidiwa na mchezaji wa zamani wa klabu hiyo, Osward Morris  walianza mchezo huo kwa kutandaza kabumbu safi hasa dakika 15 za mwanzo, lakini baadaye mambo yakawageukia kabisa na kama Ashanti wangekuwa makini kubadili nafasi muhimu za kufunga kuwa magoli, basi wangemaliza dakika 45 wakiwa kifua mbele.
Kipindi cha pili, Ashanti chini ya kocha wake, Nico Kiondo iliongeza kasi ya mashambulizi langoni mwa Prisons, lakini kukosekana kwa umakini wa washambuliaji wake kuliwagharimu na kushindwa kuweka gozi kambani.
Kwa ushindi huo, Ashanti inatimiza point nane baada ya kucheza mechi tisa na sasa inasogea hadi nafasi ya 10 kutoka ya 13.
Kikosi cha Ashanti United leo: Daudi Mwasongwe, Hussein Mkongo/Anthony Matangalu dk46, Jaffar Gonga, Tumba Sued, Samir Ruhava, Iddi Silas, Mussa Nampaka, Fakhi Hakika/Mwinyi Allydk83, Paul Maona, Joseph Mahundi na Lusajo Mwakyusa/Hussein Swedi dk51.
Prisons: Beno David, Salum Mashaka, Laurian Mpalile, Lugano Mwangama, Nurdin Issa/Frank William dk82, Omega Seme, John Matei, Freddy Chudu, Peter Michael, Hassan Isaka/Jumanne Elfadhil dk71 na Julius Kwanga/Jeremiah Juma dk47.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video