Tuesday, October 1, 2013

SONY DSCMwenyekiti wa Muungano wa Jinsia na Katiba (GFC) , Magdalena Rwebangira akiwasilisha mada wakati Warsha ya mrejesho na taarifa kwa wadau kutoka Jukwaa la Katiba ya siku moja iliofanyika Septemba 3o-2013 katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam, lengo likiwa ni kujadili rasimu ya Katiba na baadhi ya mambo yaliyojadiliwa ni haki ya kumiliki mali na kutaka Katiba iwe na kipengele kinachohusu haki sawa ya kumiliki ardhi kwa wanawake, watoto na makundi mengine maalum, ilioandaliwa na Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania TAWLA 002Mbunge wa viti maalumu Ester Bulaya (CCM, akichangia mada wakati wa Warsha ya wadau wa Jukwaa la katiba yasiku moja iliofanyika Septemba 3o-2013 katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam.SONY DSCMbunge wa viti maalumu, Ester Matiku (kulia) Mbunge wa viti maalumu, Ester Bulaya (CCM, (kushoto kwake) akiwa pamoja na Wabunge wengine walioudhuria,wakiwa kwenye Warsha ya mrejesho na taarifa kwa wadau kutoka Jukwaa la Katiba yasiku moja iliofanyika Septemba 3o-2013 katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam,lengo la Warsha hiyo ilikuwa kujadili rasimu ya Katiba na baadhi ya mambo yaliyojadiliwa ni haki ya kumiliki mali na kutaka Katiba iwe na kipengele kinachohusu haki sawa ya kumiliki ardhi kwa wanawake, watoto na makundi mengine maalum,ilioandaliwa na Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania TAWLA
…………………………………………………………………………………………………
Na Philemon Solomon wa Fullshangwe , Dar es Salaam
CHAMA cha wanasheria wanawake Tanzania (Tawla) na Wanaharakati pamoja na wabunge Wanawake wamewataka wananchi kutengeneza Katiba ya Watanzania wote na si kuegemea katika vyama au taasisi fulani pamoja na kuwa na Katiba ya inayomlinda kila mtu sanjari na kutoa mapendekezo yao.
Hayo yalizungumzwa Jijini Dare s Salaam Septemba 30-2013, na Mwenyekiti wa Muungano wa Jinsia na Katiba (GFC) Magdalena Rwebangira wakati walipokuwa wakifanya mrejesho wa taarifa kwa wadau kutoka Jukwaa la muungano wa jinsia na Katiba kwa lengo la kuhakikisha inapatikana Katiba bora kwa maslahi ya Taifa na wananchi kwa ujumla.
“Mimi ni mwanasheria lakini itafika wakati nitastaafu na sitaweza kufanya hizo kazi hivyo siwezi kutetea eti mwanasheria apewe kitu fulani au upo katika chama fulani halafu utete mpewe/kipewe kitu fulani, hivyo natamani kuweka ukurasa mpya ili kupata katiba nzuri iliyobora kwa maslahi ya taifa, alisema.
Katika warsha hiyo watu mbalimbali wakutanishwa wakiwemo wabunge na baadhi ya wananchi kutoka taasisi mbalimbali kwa lengo la kujadili rasimu hiyo ya Katiba na baadhi ya mambo yaliyojadiliwa ni haki ya kumiliki mali na kutaka Katiba iwe na kipengele kinachohusu haki sawa ya kumiliki ardhi kwa wanawake, watoto na makundi mengine maalum.
Pia walijadili haki ya usawa na utambuzi wa katiba kama sheria mama iliyo juu ya sheria zote  na kutaka iwe na kipengele kinachobatilisha sheria zote za ubaguzi wa kijinsia sanjari na kuwepo kwa kipengele kinacholinda haki na utu wa mwanamke kwa kukataza masuala unyanyasaji na ukatili wa kijinsia, ubaguzi kwa misingi ya dini, uraia, rangi, au hali ya ndoa.
Pia wadau hao walijadili suala la uwakilishi na kuitaka Katiba mpya iwe na kipengele kinachaonisha wazi kuwa nafasi za juu ya uongozi wa nchi ziwe na uwino kwa wanawake na wanaume  kwa maana rais akiwa Mwanaume Makamu wake au Waziri Mkuu awe mwanamke.
 Mbunge wa viti maalumu Ester Bulaya (CCM) mkoani Mara amewataka wabaunge kuunganisha nguvu zao katika kukaa pamoja na kutengeneza katiba Mpya na si kuanza kuyumbisha hali itakayowapa nafasi watu wa nchi ya jirani kupenyeza hila zao na kuiweka nchi pabaya kwa maslahi yao.
“Ili kupata Tanzania iliyosafi kwa miaka ijayo ni vema wabunge wote tukaonganisha nguvu zetu na kuwa kitu kimoja kabla ya kwenda katika bunge la Katiba kwa lengo la kuwa na masahisho sahihi kwa maslahi ya taifa na si kutegeana na kwenda kukomoana katika Bunge,” alisema.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video