Afisa
Habari wa klabu ya Yanga SC Baraka Kizuguto (kushoto) akiongea na
waandishi wa habari, kulia ni Lawrence Mwalusako -Kaimu Katibu Mkuu
Uongozi
wa klabu ya Young Africans leo umetangaza rasmi kuanza kwa zoezi la
kupiga kura ya NDIYO juu ya uundwaji wa kampuni au kura ya HAPANA kwa
kutoridhia klabu kuwa kampuni maazimio yaliyofikiwa katika mkutano mkuu
uliofanyika Januari 16, 2013.
Akiongea
na waandishi wa habari makao makuu ya klabu ya Yanga kaimu katibu mkuu
Lawrence Mwalusako amesema zoezi hilo linanza leo kwa wanachama hai
kufika makao makuu ya klabu na kupiga kura ya NDIYO au HAPANA na zoezi
hilo litaendelea mpaka novemba 10, 2013.
Ifuatayo ni Taarifa kwa Wanachama na Waandishi wa Habari
MAONI YA WANACHAMA YA KUUNDA KAMPUNI
Katika
Mkutano wa Kawaida wa Wanachama wa YANGA uliofanyika tarehe 16 Januari
2013 Mwenyekiti kwa niaba ya Kamati ya Utendaji aliwapa Wanachama
wafikirie mapendekezo ya YANGA kuwa Kampuni ama kutokuwa Kampuni kisha
kuyawasilisha kwa Katibu Mkuu wa YANGA.
Nachukua
nafasi hii kuwaambia Wanachama wa YANGA kuwa kuanzia leo tarehe 16
Oktoba 2013 mpaka tarehe 10 Novemba 2013, kutakuwa na sanduku moja (1)
hapa Klabuni kwa ajili ya kukusanya kura za maoni ya Wanachama ya
kuanzisha Kampuni (NDIYO) au kutokuwa Kampuni (HAPANA)
Kila
Mwanachama hai atakuwa na uhuru wa kupiga kura na atalazimika kuja na
Kadi yake ambapo itamzuia kupiga kura mara mbili au zaidi.
Zoezi hili ni muhimu kwa ajili ya maendeleo ya YANGA.
“YANGA DAIMA MBELE NYUMA MWIKO”
LAWRENCE MWALUSAKO
0 comments:
Post a Comment