Wednesday, October 2, 2013


1348863630Erni
Ernie Brandts atapambana na Mecky Mexime
Na Baraka Mpenja wa Fullshangwe, Mbeya
Wakata miwa wa mashamba ya Manungu Turiani Mkoani Morogoro, Mtibwa Sugar chini ya kocha mzalendo, Mecky Mexime wamejigamba kuwatafuna mabingwa watetezi wa ligi kuu soka Tanzania bara, klabu ya Yanga katika mchezo wao wa siku ya jumapili (Octoba 6), Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Akizungumza na Mtandao wa FULLSHANGWE, Afisa habari wa klabu hiyo mwenye tambo za kila aina, Tobias Kifaru Lugalambwike amesema wembe waliotumia msimu uliopita uwanja wa Jamhuri Morogoro ambapo Yanga walilala 3-0 ndio watakaotumia kuwamaliza Wanajangwani siku hiyo.
“Mtibwa ni timu bora kwa wakati wote, unapozungumzia soka la Tanzania huwezi kuisahau klabu hii mbali ya wakongwe Yanga na Simba, hawa wengine kama Azam fc wamekuja sasa hivi tu, sisi ni wazoefu na bora, hakika jumapili Yanga watapata shida kubwa sana”. Alisema Kifaru.
Kifaru aliongeza kuwa walisikitishwa sana na matokeo ya sare ya mabao 2-2 na vibonde Ashanti United, wiki iliyopita, lakini amekiri kuwa makosa madogo sana yaliwagharimu na kushindwa kuwafunga wadhaifu hao wa jiji.
SONY DSC
Mecky Mexime, kocha Mtibwa Sugar
“Licha ya kushindwa kuwamaliza Ashanti, kocha wetu na nahodha wa zamani wa klabu hiii na Taifa Stars, Mecky Mexime anaendelea kuwafua vijana wake na amesema lazima awaoneshe kazi Yanga wanaoingiza pesa zao nyingi uwanjani lakini kazi ndogo kweli”. Alisema Kifaru.
Afisa habari huyo alikiri kuwa Yanga ni wagumu sana hasa wakiwa Dar, lakini wataoneha makeke yao kutoka Manungu Complex, na lazima wajute na mzungu wao.
Wakati Mtibwa Sugar wataingia Uwanjani wakiwa na kumbukumbu ya kulazimishwa sare na Ashanti United wiki iliyopita katika uwanja wa Azam Complex, Yanga wao waliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting inayonolewa na kocha Mtanzania, Charles Boniface Mkwasa.
Pia katika mchezo huo, mchezaji wa zamani wa Wana TamTam, Hussein Javu ataitumikia klabu yake ya Yanga dhidi ya Mtibwa Sugar kwa mara ya kwanza kuivaa timu yake ya zamani katika michuano ya ligi kuu msimu huu, ingawa alicheza katika mchezo wa kirafiki baina ya klabu hizo kujiandaa na ligi na kufunga bao moja katika ushindi wa Yanga.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video