Kikosi cha Prisons |
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
LIGI
kuu soka Tanzania bara inatarajiwa kuendelea kesho katika dimba la Azam
Complex, Mbande, Chamazi, nje kidogo ya jiji la Dar es salaam baina ya
timu mbili zinazochuana nafasi za mwisho katika msimamo, Ashanti
United `Watoto wa jiji` dhidi ya maafande wa magereza waliojeruhiwa na
Mnyama Simba wiki iliyoipta, Tanzania Prisons `Wajelajela` kutoka jijini
Mbeya.
Katibu mkuu wa Prisons, Inspekta, Sadick Jumbe ameuambia mtandao wa MATUKIO DUNIANI
kuwa maandalizi ya mechi hiyo yamekamilika ambapo kocha mkuu Jumanne
Chale akisaidiwa na Osward Morris wamefanya marekebisho ya makosa
yaliyowagharimu jumamosi ya wiki iliyopita na kufungwa bao 1-0 na vinara
wa ligi hiyo wenye pointi 18 kibindoni, Wekundu wa msimbazi Simba Sc.
“Mechi
dhidi ya Simba tulikuwa na uwezo wa kushinda, lakini wachezaji wetu
hasa safu ya ushambuliaji walikosa nafasi kadhaa za wazi, hivyo mwalimu
Chale amekazania zaidi eneo hili la umaliziaji na kwa asilimia kuwa kazi
imekamilika na kinachosubiriwa ni mechi ya kesho dhidi ya Vipofu
waliiona mwezi baada ya kuibamiza Coastal union 2-1, ndugu zetu Ashanti
United”. Alisema Jumbe.
Wanandinga wa Ashanti wakipiga jalamba |
Jumbe
alisema wachezaji wote wapo salama na Fredy Chudu ambaye alikuwa
majeruhi, naye yupo tayari kutumika kesho, hivyo mashabiki wakae mkao
wa kupokea ushindi katika kipute hicho.
Hata
hivyo Jumbe amekiri wazi kuwa tatizo kubwa la kikosi chao ni safu ya
ushambulaiji ambayo inashindwa kufumania nyavu, lakini amesema kocha
Chale anakifua vilivyo na wanatarajia matokeo mazuri kuanzia mechi ya
kesho na mechi zajazo ikiwemo ile ya mahasimu wao wa jadi, Mbeya City
katika dimba la Sokoine jijini Mbeya siku zijazo.
“Soka
ni mchezo wa makosa, kesho tunashuka dimbani, tumejiandaa kushinda,
lakini chochote kinaweza kutokea. Mashabiki watuunge mkono kwa dhati
kwani ligi bado sana na tuna nafasi ya kushinda”. Alisema Jumbe.
Kwa
upande wao Ashanti United kupitia kwa Afsia habari wao, Marijani Rajab
wamesema sasa wameamka na kazi yao ni kutafuta pointi tatu kwa kila
mechi mbele yao.
“Watu
wanatuona kama hatuna uwezo kabisa, kumbuka tulifanya vizuri sana ligi
daraja la kwanza, wachezaji ni walewale, mechi za kwanza walikuwa na
hofu kutokana na kukosa uzoefu, lakini kwasasa wameanza kuimarika na
ndio maana timu angalau inapata matokeo”. Alisema Marijani.
0 comments:
Post a Comment