Wednesday, October 16, 2013

Zitto Kabwe(3)
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC),Zitto Kabwe
Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), imeiagiza ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, kuzuia ruzuku ya kila mwezi kwa vyama baada ya kubainika kuwa kwa miaka minne mfululizo vimekuwa vikikwepa kukaguliwa mahesabu yao.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Zitto Kabwe, alisema Sh. bilioni 67.7 zilizotolewa kwa vyama tisa kwa miaka minne iliyopita, lakini havijakaguliwa mahesabu yao.
Alitaja vyama hivyo kuwa ni Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambacho kilipewa Sh. bilioni 50.9, Chadema Sh. bilioni 9.2, CUF Sh. bilioni 6.3, NCCR-Mageuzi Sh. milioni 677, DP  Sh. milioni 3.3,  Chausta Sh. milioni 2.4, UDP  Sh. milioni 333, TLP  Sh. milioni 217 na APPT Maendeleo Sh. milioni 11.
Zitto alisema kuanzia mwezi huu vyama hivyo visipewe ruzuku ya kila mwezi ambayo imekuwa ikitolewa na serikali hadi hapo vitakapofanya ukaguzi wa mahesabu na kuyawasilisha kwa ofisi ya msajili.
Alisema fedha hizo ni nyingi na zinatolewa na serikali na kwamba kwa muda wa miaka minne vyama vimekuwa vikikwepa kukaguliwa huku vikitoa visingizio mbalimbali.
Alifafanua kuwa kabla ya mwaka 2009, vyama hivyo vilikuwa vinatafuta wakaguzi wao binafsi, lakini baada ya hapo utaratibu ulibadilika na kutakiwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kufanya kazi hiyo.
Alisema atawaita makatibu wakuu wa vyama vyote ili wajieleze kwa nini hawakukaguliwa mahesabu yao kwa kipindi chote hicho huku wakiendelea kupokea ruzuku ya serikali kwa kila mwezi.
“Ukaguzi huu ni muhimu sana na kila chama lazima kihakikishe kinakaguliwa na ripoti kupelekwa kwa msajili wa vyama vya siasa kwa sababu fedha hizi ni za serikali,” alisema.
Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, alithibitisha kwamba ofisi yake haijapokea mahesabu ya vyama hivyo na kwamba ukaguzi huo ni lazima ufanywe na vyama kwa mujibu wa sheria.
CHANZO: NIPASHE

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video