Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail
BEKI
wa washika bunduki wa kaskazini mwa London, klabu ya Arsenal, Thomas
Vermaelen amekiri kuwa ataanza kufikiria hatima yake ya baadaye klabuni
hapo kama atashindwa kuingia kikosi cha kwanza cha Arsene Wenger.
Beki huyo wa kati aliyeanza katika kikosi cha timu yake ya Taifa ya
Ubelgiji dhidi ya Wales mjini Brussels jumanne ya leo alisema ataanza
kuangalia kwa umakini maamuzi yake ya kubaki au kuondoka kama ataendelea
kuanzia benchi Emirates, kwani siku zote mchezaji mwenye kipaji kama
yeye hapaswi kuwa nje ya kikosi cha kwanza.
Kikosi
cha Ubelgiji kilifuzu kwa mara ya kwanza kucheza fainali za kombe la
dunia mwakani baada ya ukame wa miaka 12 siku ya ujumaa ya wiki
iliyopita baada ya kushinda mbele ya Croatia.
Safari
hiyo ya Brazil tayari imeingia kichwani mwa beki huyo wa kati na sasa
anafikiria nafasi yake ya kucheza kikosi cha kwanza cha timu yake ya
Asernal ili kumshawishi kocha mkuu wa timu ya Taifa yake ya Taifa, Marc
Wilmots kumfikiria katika safari hiyo ya mafanikio.
Alipoulizwa
nafasi yake Emirates, Vermaelen alisema: ‘Natakiwa kuliwaza hilo pale
itakapobidi. Imebaki miezi michache kufikia januari. kiukweli, kutocheza
kamwe hakutanisaidia katika safari yangu ya kucheza fainali za kombe la
Dunia mwakani Brazil”.
“Watu wananiuliza kama sichanganyikiwi wakati huu ambao sichezi sana, lakini haiko hivyo”.
Mzee wa kusugua benchi: Nahodha wa Arsenal,Vermaelen amepoteza nafasi ya kuanza kikosi cha kwanza klabuni kwake
Anapambana katika klabu yake na timu yake ya Taifa ya Ubelgiji ili kulinda nafasi yake.
Vermaelen amepoteza nafasi hiyo na kumuacha kocha wake, Arsene Wenger kuwatumia zaidi Laurent Koscielny na Per Mertesacker.
Hata
katika kikosic cha Ubelgiji bado ana kazi kubwa ya kugombania nafasi na
wachezaji wakali ambao ni Vincent Kompany na Jan Vertonghen.
Majukumu ya kimataifa: Vermaelen akiwasili katika mazoezi ya Ubellgiji sambamba na nyota wa Tottenham, Jan Vertonghen
Wanasugua
benchi: Vermaelen (mstari wa nyuma kushoto) akiwa amekaa benchi na
Nicklas Bendtner na Nacho Monreal, huku naye Jack Wilshere mstari wa
mbele akiwa anasugua katika adimba la Emirates
0 comments:
Post a Comment