JESHI
la polisi jijini Mbeya limesema kamwe halikubaliani na vurugu
zinazojitokeza kwa mashabiki wa kandanda mkoani humo katika michezo
mbalimbali ya ligi kuu soka Tanzania bara na ligi nyingine.
Kamishina
msaidizi wa Polisi ambaye pia ni mkurugenzi wa kitengo cha upelelezi
mkoani Mbeya na Kaimu kamanda wa polisi, Robert Mayala ameuambia mtandao
wa MATUKIO DUNIANI kuwa juzi mashabiki wanaosadikika kuwa wa Mbeya
City walishambulia gari za Tanzania Prisons eneo la Hoteli ya Rift
Valley wakati wanarudi kambini na kupasua vioo sanajari na kuwajeruhi
baadhi ya wachezaji akiwemo Lugano Mwangamba.
“Michezo
ni furaha na sio vurugu, mashabiki wa Mbeya City hawakuwa na sababu ya
kufanya vurugu kwani walikuwa wameshinda mchezo huo, na mpaka kufikia
jana watu sita tunawashikilia na leo hii (jana) tunawapeleka mahakamani
kusomewa mashitaka. Kwa pamoja tunalaani vurugu hizi na tunaahidi
kuchukua hatua kali”. Alisema Kamishina msaidizi wa Polisi Robert
Mayala.
Kamishina
msaidizi Mayala aliongeza kuwa Kushambulia wachezaji au mashabiki ni
kosa kama makosa mengine kisheria, na wao watahakikisha wanaohusika
wanafikishwa mbele ya vyombo vya dola.
“Kama
tutaliachia hili kuendelea kutokea, watu wengi wataacha kwenda
viwanjani kushuhudiwa mpira, na tutapotosha zana halisi ya mpira ambao
siku zote ni burudani na amani”. Alisema Kamishina Mayala.
Wakati
jeshi la polisi likisema hilo, tayari uongozi wa Tanzania Prisons,
`Wajelajela` kupitia kwa katibu wake mkuu, Inspeckta Sadick Jumbe
wameeleza kusikitishwa na vitendo walivyofanyia na baadhi ya mashabiki
wa Mbeya City.
Jumbe
alisema wao wameshakubali matokeo bila tatizo lolote, lakini
hawakubaliani na vurugu walizofanyiwa, hivyo wamesema wanaandika
ushahidi wa kimaandishi ambao watawasilisha shirikisho la soka nchini
Tanzania TFF.
“Kama
Mbeya City wamefikia hatua ya kutufanyia vurugu ndugu zao, je,
itakuwaje kwa wageni?, Waliwafanyia vurugu wakongwe Yanga, jana (juzi)
sisi, na Ashanti wanakuja Mbeya, hawatawafanyia vibaya zaidi?. Alihoji
Jumbe.
Vioo nyang`anyang`a: Gari la Wajelajela Tanzania Prisons lilipigwa mawe na baadhi ya wachezaji kujeruhiwa
Inspeckta
huyo alisema ana uwezo kisheria wa kuwaruhusu vijana wakapambana na
watu hao, lakini kama akifanya hivyo atafanya mambo yawe mabaya kwa
wapinzani wao kwani nguvu wanazo na uwezo wa mapambano kijeshi wanao.
“Nitoe
rai kwa Mheshimiwa Rais wa TFF, Jamal Emily Malinzi kuanza uongozi wake
kwa kuwachukulia hatua kali Mbeya City, wao tu ndio wanapenda vurugu.
Ipo siku hatutawavumilia”. Alisema Inspecta Jumbe.
Nao
Mbeya City kupitia kwa katibu wake mkuu, Emmanuel Kinde wamekanusha
kuhusika na tukio hilo, bali amesema kuwa ni mpango uliopangwa na
Prisons ili kufanya vurugu.
Kinde
alisema awali walikaa na jeshi la polisi na kukubaliana kuwa mwisho wa
mechi timu zote zisindikizwe na polisi, lakini haikuwa hivyo.
Pia walisikia kuwa kuna watu wana mpango wa kufanya vurugu na waliwaambia polisi, lakini hawakulichukulia uzito.
“Sisi
tunajua Prisons wanaeneza propaganda zao ili wahame Mbeya, ni mpango wa
muda mrefu wa kutaka kuuhama uwanja wa Sokoine, wao waondoke na sisi
tutabaki. Na ninavyokuambia hivi , kuna watu wamekamatwa sehemu tofauti
kabisa na uwanjani kwa kwa madai ya kuhusika na vurugu na wanapelekwa
mahakamani kesho (leo)’. Alisema Kinde.
Kinde
aliongeza kuwa ni wakati wa matatizo ya mpira kutatuliwa kwa misingi ya
kimpira, hivyo amewataka mashabiki wao kuwa watulivu wakati huu, pia
ametoa wito kwa watu wa usalama kuwa makini na upotoshwaji wa Taarifa.
0 comments:
Post a Comment