Moja
ya soko maarufu hapa mjini mpanda ambalo ni tegemeo kwa wakazi wa mjini
mpanda hususani wakazi wa majengo. soko hilo liko majengo mapya kata
ya KawanjeseH/Mji wa Mpanda, pia so limezungukwa na uchafu kila kona
huku pembeni kukiwa na Dampo la kumwanga uchafu eneo ambalo siyo rasmi
na mamlaka husika kila siku zinapita na kuuangalia, na mbaya zaidi soko
hilo liko mbele ya ofisi ya mtendaji wa kata, mtaa wa kawajense na
ofisi ya afisa afya ngazi ya kata anaangalia bila kuchukua hatua zozote
za kutoe elimu kwa jamii na pengine sheria ichukue mkono wake.
Dampo
la kutupia uchafu likiwa mbele ya soko la kuuzia mboga mboga na vyakula
aina ya matunda katika mji wa mpanda eneo la kawajense hali ambayo ni
hatari kwa watumiaji wa vyakula kutoka katika soko hilo. Na
iwapo hatua za makusudi hazitachuliwa kuthibiti hali hiyo hasa wakati
tunapoelekea kuanza kunyesha kwa msimu wa mvua ni hatari kwa wananchi
kwani wanaweza kukumbwa na magonjwa ya mlipuko kama kuhara, kipindupindu
na matokeao yake kupoteza maisha.
Hali ya kuzingatia usafi ni jukumu la mamlaka husika kuliangalia kwa
mapana na marefu na kuchukua hatua za makusudi kuelimisha jamii kabla ya
kutokea madhara zaidi. Heri kuzuia kuliko kutibu, kazi kwenu wenye
dhamana.

Mama
na Mwana wakijitafutia riziki kwa kuchoma mkaa na kujikuta
wakijihusisha na ukataji wa miti kiholela, kiukweli, kama tabia hii
itazidi kushika kasi zaidi na zaidi, Mpanda wanakaribisha ukame huku
wakijiona kabisa. Suala la utunzaji wa mazingira ni kuanzia kwa wananchi
ambao wanapaswa kuelemishwa na kukumbushwa, hadi mamlaka zinazohusika,
`Tunza mazingira yakutunze`.

Uharibifu
wa mazingira unachangiwa na mambo mengi na pengine umasikini na
kutokuwa na uelewa wa kutosha kutokana na athari za uharibifu huo hasa
umasikini kama mama huyo ambaye jina lake halikuweza kufahamika akiwa na
mwanaye wakichoma tanuru la mkaa ili kujitafutia riziki, mkono uweze
kwenda kinywani kwa kuwa hana jnsi nyingine ya kupata kipato badala yake
anategemea kuchoma mkaa kama alivyokutwa na kamera katika kijiji cha
Sungamila Kat ya Kasokolo H/Wilaya ya Nsimbo Wilaya ya Mlele.
PICHA NA KIBADA WAKIBADA-MPANDA-KATAVI
0 comments:
Post a Comment