Na Baraka Mpenja wa Fullshangwe, Mbeya
Shirikisho la soka Tanzania, TFF limewaonya na kuwakataza mashabiki wa soka nchini kuacha mara moja tabia ya kuingia na silaha uwanjani wakati wa mechi za ligi kuu soka Tanzania bara.
Afisa habari wa TFF, Boniface Wambura Mgoyo amesema kuwa kanuni za usalama za FIFA zinaeleza wazi kuwa ni marufuku kwa shabiki yeyote kuingia uwanjani na silaha ya aina yoyote wakati wa mechi.
“FIFA katika sheria zake za usalama, inasema kuwa silaha hazitakiwi uwanjani, hivyo ni kosa kwa mashabiki kuingia na silaha kwa sababu zozote zile, lakini mechi za wikiendi iliyopita imebainika kuwa kuna watu waliingia na silaha na kukamatwa na Polisi”. Alisema Wambura.
Wambura alifafanua kuwa katika mechi ya jumamosi iliyopita baina ya Yanga na Ruvu Shooting, mashabiki 11 walikamatwa na silaha aina ya Bastola, wakati katika mchezo wa Simba Sc na JKT Ruvu uwanja huo wa Taifa, mashabiki 6 walikamatwa na silaha aina hiyo.
Kwahiyo mashabiki 17 walikamatwa na Bastola Uwanja wa Taifa na hali hii inatakiwa kupigwa vita mapema kwani ni hatari sana.
Wote waliokutwa na silaha hizo walikuwa na leseni za kuzimiliki.
Hivyo, kwa washabiki wanaomiliki silaha hatawaruhusiwa kabisa kuingia viwanjani, na badala yake wanashauriwa kuzihifadhi huko wanakotoka kabla ya kufika viwanjani.
Pia TFF inatoa mwito kwa shabiki ambaye atamuona mwenzake akiwa na silaha uwanjani kutoa taarifa kwa mamlaka husika likiwemo Jeshi la Polisi ili aweze kuchukuliwa hatua.
Wakati huo huo; Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inaingia raundi ya saba kesho (Oktoba 5 mwaka huu) kwa mechi nne ambapo Ruvu Shooting itakuwa mwenyeji wa vinara Simba kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Viingilio katika mechi hiyo itakayochezeshwa na mwamuzi Mohamed Theofil kutoka Morogoro kuanzia saa 10 kamili jioni vitakuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000. Tiketi zitauzwa uwanjani kuanzia saa 4 asubuhi.
Mechi nyingine za kesho ni JKT Ruvu itakayoumana na Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam huku Coastal Union ikiwa mwenyeji wa Azam kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid jijini Arusha ndiyo utakaotoa fursa kwa timu za Oljoro JKT na Mbeya City kuoneshana ujuzi katika kusaka pointi tatu.
Ligi hiyo itaendelea Jumapili (Oktoba 6 mwaka huu) kwa mechi kati ya Yanga na Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati Mgambo Shooting itaialika Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

0 comments:
Post a Comment