Tegete
ndiye mchezaji wa Yanga aliyemfunga mara nyingi kipa wa Simba
aliyecheza mechi nyingi za watani wa jadi, Juma Kaseja ambaye alitemwa
na Simba kabla ya kuanza Ligi Kuu ya msimu huu.
………………………………………………………………………………………………
JERRY Tegete anaingia kwenye mechi ya watani wa jadi Jumapili akiwa na faida moja.
Ndiye mchezaji pekee aliyefunga mabao mengi kwenye mchezo baina ya timu hizo katika kipindi cha miaka 10.
Amri Kiemba wa Simba amefunga mabao mawili kwenye msimamo wa wafungaji wa watani wa jadi ndani ya miaka hiyo 10.
Wafungaji Bora kwa miaka 10
kwenye michezo kati ya Simba na Yanga ni Emmanuel Gabriel na Mussa Mgosi
wote walikuwa Simba na wana mabao matano. Wenye mabao manne ni Jerry
Tegete (Yanga) na Nico Nyagawa (Simba).
Haruna Moshi’Boban’ (Simba) ana
mabao matatu wakati wenye mabao mawili ni Kiemba (alifunga akiwa Yanga
kisha Simba), Athumani Machupa (Simba), Credo Mwaipopo (Yanga),
Emmanuel Okwi (Simba), Herry Morris (Yanga), Hillary Echesa (Simba) na
Kudra Omary (Yanga).
Katika orodha hiyo Kiemba na
Tegete tu ndio waliosalia kwenye timu hizo mpaka sasa huku wengine
wakistaafu soka na baadhi kuhamia timu nyingine.
Tegete
ndiye mchezaji wa Yanga aliyemfunga mara nyingi kipa wa Simba
aliyecheza mechi nyingi za watani wa jadi, Juma Kaseja ambaye alitemwa
na Simba kabla ya kuanza Ligi Kuu ya msimu huu.
CHANZO: MWANASPOTI
0 comments:
Post a Comment