Madereva na Mafundi wa Treni za TAZARA wakiwa katika moja ya vichwa sita vipya vya Treni ambavyo vimeletwa Tanzania na wapo katika mafunzo ya jinsi ya kuvitumia. (Picha na Furaha Eliab, Mbeya)
Na Furaha Eliab, Mbeya
SHIRIKA la reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) limepata vichwa sita vya Treni vipya kutoka nchini China vyenye uwezo wa kubeba tani 1800 kila kimoja.
Kufuatia kutolewa kwa vichwa hivyo vya Treni vipya, madereva 160 na mafundi 80 wa karakana ya Treni Iyunga mkoani Mbeya wanapatiwa mafunzo yakakayo wawezesha kufanya kazi kwa umakini katika vichwa hivyo.
Akitoa maelezo ya ujio wa vyicho hivyo Mhandisi Mwandamizi katika karakana na Iyunga Eng. Davie Tembo alisema kuwa vichwa hivyo vya treni vyenye uwezzo wa kubeba Tani 1800 vimeletwa Juzi katika karakana hiyo.
Alisema kuwa vimetoka nchini china na ni toleo jipya ambalo linahitaji madereva na mafundi kujifunza kabla ya kuanza kutumia kwani linatumia mfumo mpya.
Tembo alisema kuwa kampuni ya CSR Qishuyan ya nchini China ndio iliyo tengeneza vichwa hivyo na inatoa mafunzo kwa madereva na mafundi jinsi ya kuvimudu vichwa hivyo.
Alisema kuwa wamevijaribu vichwa hivyo na kuviona vinafaa kwa matumizi na havina shida yoyote.
Awali akifungua mafunzo kwa madereva hao Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa TAZARA, Said Sauko alisema kuwa mafunzo hayo yatalenga kwa Wafanyakazi wa TAZARA watakao kuwa katika makundi saba ambapo kila kundi litakuwa na watu wasio pungua 40.
Alisema kuwa mafunzo hayo yatatolewa kwa muda wa mwezi mmoja na yamelenga kwa wafanyakazi kutoka Tanzania na Zambia.
0 comments:
Post a Comment