Jeshi
la Polisi Tanzania linawaita kwenye usaili wahitimu wa vyuo vya Elimu
ya Juu na vya Ufundi Stadi ambao majina yao yanapatikana katika tovuti
ya Jeshi la Polisi Tanzania, www.policeforce.go.tz
Orodha ya majina hayo itapatikana pia katika Gazeti la habari Leo la tarehe 04/11/2013.
Usaili
utafanyika kuanzia tarehe 11/11/2003 hadi tarehe 15/11/2013 saa mbili
asubuhi [02:00] hadi saa kumi jioni [10:00] kila siku kwa taaluma/fani
na katika maeneo yafuatayo;
· Fani
za Menejimenti ya Rasilimali Watu, Utawala, Uchumi, Usimamizi wa
Sheria na Utekelezaji(BaLe), Ualimu, Sosholojia, Saikolojia na Ushauri
Nasihi, Sheria, Takwimu, Lugha, Uhusiano wa Kimataifa, Uandishi wa
habari na Mawasiliano ya Umma, Maendeleo ya Jamii, Ukutubi na Utunzaji
Kumbukumbu. Usaili wa fani hizi utafanyika katika chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam(DPA) kilichopo kando kando ya barabara ya Kilwa Kurasini Dar es salaam .
· Fani
ya Udereva ,Ufundi rangi za magari(spray and Painting /Panel Beating ),
Ufundi wa matengenezo ya Magari Makubwa(Auto-Mechanics-Heavy Duty) na
Ufundi wa Matengenezo ya Umeme wa Magari(Auto Elecrical ). Usaili wa
fani hizi utafanyika Kikosi cha Polisi Ufundi kilichopo kando kando ya barabara ya Kilwa Kurasini Dar es salaam.
· Fani za Kompyuta. Usaili wao utafanyika nyuma ya kikosi cha Ufundi yaani TEHAMA KEKO chini.
- Fani ya Uhandisi Mitambo(Mechanical Engineering ). Usaili wao utafanyika Kikosi cha Polisi Anga kilichopo Uwanja wa Ndege JK Nyerere DSM.
- Wataalam wa masuala ya Afya/Wauguzi usaili wao utafanyika katika kikosi cha afya kilichopo kando kando ya barabara ya Kilwa Kurasini Dar es salaam.
Muhimu:
(i)Mwombaji
afike kwenye usaili akiwa na nakala halisi pamoja na vivuli vya
vyeti vyote vya Masomo/Taaluma [Academic Transcript
(s)/Certificate(s)]yaani kidato cha nne, sita ,Chuo na cheti cha
kuzaliwa. Hati ya kiapo cha kuzaliwa haitakubalika.
(ii)Mwombaji
aliyeitwa kwenye usaili atalipia gharama za upimaji afya shilingi elfu
kumi (10,000), usafiri, chakula na malazi kwa muda wote wa zoezi la
usaili.
(iii)Kwa
kuwa muda ni mchache anaekuja kwa usaili ajiandae baada ya usaili
atakaechaguliwa atapelekwa katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Moshi siku
nne baada ya usaili kwisha yaani tarehe 19/11/2013.
0 comments:
Post a Comment