WILAYA YA MBARALI – AJALI YA PIKIPIKI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU NA
KUSABABISHA KIFO NA MAJERUHI.
KUSABABISHA KIFO NA MAJERUHI.
MNAMO
TAREHE 22.10.2013 MAJIRA YA SAA 15:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA
MKOMBWE, KATA YA UBARUKU, TARAFA YA RUJEWA, WILAYA YA MBARALI MKOA
WA MBEYA. PIKIPIKI T.656 BDG AINA YA LIFAN IKIENDESHWA NA WAKATI S/O
CHARLES, MIAKA 22, MBUNGU, MKAZI WA MKOMBWE, LILIMGONGA MTEMBEA KWA
MIGUU MTOTO AGREY S/O MPWEPWA, MIAKA 5, MSANGU, MKAZI WA KIJIJI CHA
MKOMBWE NA KUSABABISHA KIFO CHAKE WAKATI ANAPATIWA MATIBABU HOSPITALI
YA MISHENI RUJEWA AMBAYE MWILI WAKE UMEHIFADHIWA HOSPITALINI HAPO.
AIDHA KATIKA AJALI HIYO MWENDESHA PIKIPIKI ALIJERUHIWA NA AMELAZWA
KATIKA HOSPITALI HIYO, TARATIBU ZA KISHERIA ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE
MAHAKAMANI. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA
MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA
MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA
NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
WILAYA YA MBARALI – AJALI YA GARI KUGONGA GARI NYINGINE KWA NYUMA NA
KUSABABISHA KIFO NA MAJERUHI.
KUSABABISHA KIFO NA MAJERUHI.
MNAMO
TAREHE 22.10.2013 SAA 19:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA MACHIMBO, KATA YA
UJELELE, TARAFA YA RUJEWA, BARABARA YA MBEYA/IRINGA WILAYA YA
MBARALI MKOA WA MBEYA. GARI T.964 AUN/T.730 BPL AINA YA SCANIA TANKI
LIKIENDESHWA NA DEREVA SAMORA S/O PETER, MIAKA 35, MHEHE, MKAZI WA
DSM, LILIGONGA KWA NYUMA GARI T.641 AQQ/ T.935 AUV AINA YA SCANIA
LIKIENDESHWA NA DEREVA ALLY S/O SALIM, MIAKA 38, MPARE MKAZI WA DSM NA
KUSABABISHA KIFO UTINGO WA GARI T.964 AUN/T.730 BPL ALIYEFAHAMIKA KWA
JINA MOJA LA HAMAD S/O ? NA MAJERUHI KWA DEREVA SAMORA S/O PETER AMBAYE
AMELAZWA HOSPITALI YA MISHENI CHIMALA, TARATIBU ZA KISHERIA ZINAFANYWA
ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI WA GARI
T.964 AUN/T.730 BPL. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA
MISHENI CHIMALA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA
POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA
VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI
KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
WILAYA YA CHUNYA – KUPATIKANA NA NYARA ZA SERIKALI
[ DIWANI ATHUMANI - ACP ]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
0 comments:
Post a Comment