![]() |
[DIWANI ATHUMANI - ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA. |
“PRESS RELEASE” TAREHE 19. 10. 2013.
WILAYA YA RUNGWE – MAUAJI.
MNAMO
TAREHE 18.10.2013 MAJIRA YA SAA 18:30HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA KIKOTA
,KATA YA KIWIRA TARAFA YA UKUKWE WILAYA YA RUNGWE MKOA WA MBEYA. GOD
S/O ADAMU, MIAKA 20, KYUSA, MKULIMA, MKAZI WA JIJINI MBEYA, ALIUAWA
BAADA YA KUPIGWA NA KUNDI LA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA
MKONONI WAKITUMIA SILAHA ZA JADI MAWE NA MAGONGO KISHA MWILI WAKE
KUCHOMWA MOTO. CHANZO NI TUHUMA ZA WIZI WA PIKIPIKI T.827 CKB AINA YA
KINGLION ALIYOIIBA NYUMBANI KWA BABA YAKE MDOGO NICODEMUS S/O JACKSON
MWALUPASO, SIKU YA TAREHE 17.10.2013 MAJIRA YA SAA 08:00HRS NA
KUIFICHA PIKIPIKI HIYO KWENYE NYUMBA AMBAYO HAIJAMALIZIKA [PAGALE].
MSAKO MKALI DHIDI YA WAUAJI UNAENDELEA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANAENDELEA KUTOA WITO KWA
JAMII KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KINYUME CHA
SHERIA, NA BADALA YAKE WAHAKIKISHE WANAWAFIKISHA KATIKA MAMLAKA HUSIKA
WATUHUMIWA WANAOWAKAMATA KWA TUHUMA MBALIMBALI ILI HATUA ZA KISHERIA
DHIDI YAO ZICHUKULIWE.
WILAYA YA MBOZI – KUPATIKANA NA SILAHA BILA KIBALI.
MNAMO
TAREHE 19.10.2013 MAJIRA YA SAA 01:30HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA
MAGAMBA, KATA YA ISANSA, TARAFA YA IGAMBA WILAYA YA MBOZI MKOA WA
MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA/MSAKO WALIMKAMATA SELIDA D/O TUSENJE,
MIAKA 32, MNYIHA, MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA IGAMBA AKIWA NA
SILAHA/BUNDUKI MOJA AINA YA S/GUN BILA KIBALI.MBINU NI KUIFICHA SILAHA
HIYO NDANI YA CHUMBA ANACHOLALA. TARATIBU ZA KISHERIA ZINAFANYWA ILI
AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI
WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUMILIKI SILAHA
BILA KUFUATA UTARATIBU KWANI NI KOSA LA JINAI. AIDHA ANAENDELEA KUTOA
RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA MTU/WATU AU KIKINDI KINACHOMILIKI
SILAHA BILA KIBALI /TENGENEZA SILAHA AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI
WAHUSIKA WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.
Signed by:
[DIWANI ATHUMANI - ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
0 comments:
Post a Comment