“PRESS RELEASE” TAREHE 17. 10. 2013.
WILAYA YA MBOZI – MAUAJI.
MNAMO
TAREHE 16.10.2013 MAJIRA YA SAA 22:30HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA MAHENJE
KATA YA MYOVIZI, TARAFA IYULA, WILAYA YA MBOZI MKOA WA MBEYA. MTU
MMOJA ASIYEFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE, JINSI YA KIUME, UMRI KATI
YA MIAKA 20-25, ALIKUTWA AMEUAWA NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA KISHA
MWILI WAKE KUTUPWA KWENYE SHAMBA MALI YA FRIDAY S/O BUKUKU. CHANZO
KINACHUNGUZWA. MWILI WA MAREHEMU ULIKUTWA NA JERAHA UBAVU WA KULIA,
UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA WILAYA YA MBOZI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA
MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA
YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA MTU/WATU WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILI
AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO
WAKE.
WILAYA YA MBOZI – MAUAJI.
MNAMO
TAREHE 16.10.2013 MAJIRA YA SAA 02:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA
ISALALO, KATA YA MSIA, TARAFA YA IGAMBA WILAYA YA MBOZI MKOA WA MBEYA.
TUSAMALE S/O MWILEGA, MIAKA 70, MNYIHA, MKULIMA, MKAZI WA ISALALO
ALIFARIKI DUNIA AKIWA AMELALA NDANI YA NYUMBA YAKE BAADA YA MTU/WATU
WASIOFAHAMIKA KUCHOMA MOTO NYUMBA YAKE. MAREHEMU ALIKUWA ANAISHI PEKE
YAKE KATIKA NYUMBA HIYO ILIYOJENGWA KWA MATOFALI MABICHI NA KUEZEKWA KWA
KUTUMIA NYASI. CHANZO KINACHUNGUZWA. MWILI WA MAREHEMU UMEFANYIWA
UCHUNGUZI NA KUKABIDHIWA NDUGU KWA MAZISHI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA
MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA
YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA MTU/WATU WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILI
AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO
WAKE.
|
Signed by:
[DIWANI ATHUMANI - ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
0 comments:
Post a Comment