“PRESS RELEASE” TAREHE 15. 10. 2013.
WILAYA YA MBEYA VIJIJINI – MAUAJI.
MNAMO
TAREHE 14.10.2013 MAJIRA YA SAA 13:30HRS HUKO KATIKA MSITU WA IHONDO
KIJIJI CHA MALANGALI KATA YA SWAYA MPAKANI MWA WILAYA YA MBEYA VIJIJINI
NA WILAYA YA RUNGWE MKOA WA MBEYA. MICHAEL S/O WILLIAD, MIAKA 24,
MSAFWA, M/BIASHARA, MKAZI WA MALANGALI WILAYA YA RUNGWE, ALIKUTWA
AMEUAWA KWA KUKATWA MAPANGA KICHWANI NA MWILI WAKE KUTUPWA KATIKA MSITU
WA IHONDO NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA. MBINU ILIYOTUMIKA NI KUMVIZIA
MAREHEMU AKIWA ANATOKA MBEYA MJINI KUNUNUA MAHITAJI/BIDHAA NDOGO NDOGO
ZA DUKANI KWAKE AKIWA NA PIKIPIKI YAKE T.819 CDQ AINA YA T-BETTER NA
KUMUUA KISHA KUMTUPA MSITUNI. PIKIPIKI YA MAREHEMU ILIKUTWA NJIANI
IMEEGESHWA IKIWA NA BIDHAA ALIZOKUWA AMENUNUA. CHANZO KINACHUNGUZWA. KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI
ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA MTU/WATU WALIOHUSIKA
KATIKA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA SHERIA
ICHUKUE MKONDO WAKE.
WILAYA YA MBARALI – AJALI YA GARI KUMGONGA MPANDA BAISKELI NA
KUSABABISHA KIFO NA MAJERUHI.
KUSABABISHA KIFO NA MAJERUHI.
MNAMO
TAREHE 14.10.2013 MAJIRA YA SAA 07:15HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA META –
IGURUSI BARABARA YA MBEYA/IRINGA WILAYA YA MBARALI MKOA WA MBEYA. GARI
T.404 AAT AINA YA TOYOTA MARK II LIKIENDESHWA NA DEREVA SAAD S/O
MWATOVENE, MIAKA 71, MSANGA, MKAZI WA CHIMALA LILIMGONGA MPANDA BAISKELI
REHEMA D/O KUNDAMA, MIAKA 21, MHEHE, MKULIMA, MKAZI WA MAPUNGA –
IGURUSI NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO NA MAJERUHI KWA ABIRIA WAKE
DANIEL S/O GEORGE, MIAKA 21, MUWANJI, MKULIMA, MKAZI WA IGURUSI AMBAYE
AMELAZWA HOSPITALI YA CHIMALA- MISHENI NA MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA
HOSPITALINI HAPO. CHANZO NI MWENDO KASI. MTUHUMIWA AMEKAMATWA TARATIBU
ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI
ATHUMANI ANAENDELEA KUTOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA
VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI
KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
WILAYA YA CHUNYA – KUPATIKANA NA BHANGI.
MNAMO
TAREHE 14.10.2013 MAJIRA YA SAA 10:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA
MAKONGOLOSI WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA
DORIA/MSAKO WALIMKAMATA RAMADHAN S/O JUMA, MIAKA 31, MSUKUMA, MKULIMA,
MKAZI WA MAKONGOLOSI AKIWA NA BHANGI DEBE MOJA SAWA NA UZITO WA KILO 10.
MTUHUMIWA NI MUUZAJI NA MTUMIAJI WA BHANGI. TARATIBU ZINAFANYWA ILI
AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA
MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANAENDELEA KUTOA WITO KWA JAMII
KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI
KWA AFYA YA MTUMIAJI.
WILAYA YA CHUNYA – KUPATIKANA NA SILAHA [RIFFLE].
MNAMO
TAREHE 13.10.2013 MAJIRA YA SAA 14:00HRS HUKO KATIKA HIFADHI YA TAIFA
YA LUKWATI WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA
DORIA/MSAKO KWA KUSHIRIKIANA NA MAAFISA WA HIFADHI HIYO WALIMKAMATA
SAMOLA S/O DAMAS, MIAKA 41, MBUNGU, MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA GUA
AKIWA NA SILAHA BUNDUKI AINA YA RIFFLE NA RISASI MBILI [02]. TARATIBU
ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANAENDELEA KUTOA WITO KWA
JAMII KUACHA TABIA YA KUJIMILIKISHA SILAHA KINYUME CHA SHERIA NA BADALA
YAKE WAFUATE TARATIBU ZILIZOWEKWA.
WILAYA YA MBEYA VIJIJINI – KUFA MAJI.
MNAMO
TAREHE 14.10.2013 MAJIRA YA SAA 13:30HRS HUKO MTO MBALIZI WILAYA YA
MBEYA VIJIJINI MKOA WA MBEYA. MTOTO AITWAYE YUSUPH S/O TIMOTH, MIAKA 12,
KYUSA, MWANAFUNZI WA DARASA LA TANO [05] SHULE YA MSINGI IWINDI
ALIFARIKI DUNIA KATIKA MTO HUO WAKATI ANAOGELEA. UCHUNGUZI WA AWALI
UMEBAINI KUWA MAREHEMU ALIKUWA AKISUMBULIWA NA TATIZO LA KIFAFA HALI
ILIYOSABABISHA KIFO CHAKE WAKATI AKIOGELEA. MWILI WA MAREHEMU
UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI TEULE YA WILAYA – IFISI. KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI
ANATOA WITO KWA WAZAZI/WALEZI KUWA MAKINI NA WATOTO WAO ILI KUWEZA
KUEPUKA MADHARA/MATATIZO YANAWEZA KUWAPATA WATOTO WAO. AIDHA ANATOA WITO
KWA WAZAZI/WALEZI WAISHIO MAENEO YENYE VYANZO VYA MAJI KUCHUKUA
TAHADHALI KWA WATOTO WAO ILI KUEPUKA MADHARA YANAYOWEZA KUEPUKIKA.
Signed by:
[DIWANI ATHUMANI - ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
0 comments:
Post a Comment