Na Baraka Mpenja
Ligi kuu soka Tanzania bara imeendele leo kushika kasi, huku mechi iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu baina ya vinara, Wekundu wa Msimbazi Simba dhidi ya maafande wa Ruvu Shooting katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam ambapo mnyama alikuwa ugenini umemalizika kwa matokeo ya ya sare ya 1-1.
Kwa matokeo hayo bado Simba anabakia kileleni akiwa na pointi 15 , lakini amepunguzwa kasi leo kinyume na matarajio ya makocha wake, Abdallah Athmani Seif `king kibadeni Mputa` na Jamhuri Kiwhelo `Julio` pamoja na mashabiki waliojua watapata mteremko wa kupata pointi tatu muhimu.
Ruvu Shooting ndio walikuwa wa kwanza kuandika bao la kuongoza kupitia kwa nyota wake Hassan Dilunga baada ya kuwazidi maarifa mabeki wawili wa Simba Sc, Mganda, Joseph Owino Gella na Mrundi, Gilbert Kaze.
Hamis Tambwe dakika ya 52 alifunga bao lake la 7 kwa njia ya mkwaju wa penati baada ya Betram Mwombeki kufanyiwa madhambi na kufanya ubao wa matangazo uliokuwa unaoneshwa kwa umakini na Azam Tv kupitia kituo cha Taifa cha TBC1 (kwa wale ambao hawakufika uwanjani) kusomeka 1-1.
Mrundi, Amis Tambwe anazidi kung`ara, leo katupia tuta lingine leo, Simba sc wakilazimisha sare ya 1-1 Ugenini dhidi ya Ruvu Shooting Uwanja wa TaifaWachezaji wa Mbeya City wakishangilia bao leo uwanja wa Sh. Amri Abeid jijini Arusha
Huko Arusha wenyeji wa Uwanja wa Sh. Amri Abeid, maafande wa JKT Oljoro walikuwa wenyeji wa Mbeya City ambao wana kauli mbio yao ya “Obejective to win” yaani kwa tafsiri isiyorasmi “Malengo ni ushindi tu”.
Mechi hiyo kali imemalizika kwa wakali wa Juma Mwambusi wanaotabiriwa kurejesha enzi za Tukuyu Stars, na Meco wakiibuka na ushindi wa pili wa mabao 2-1 na kuifanya timu hiyo ipate ushindi wa pili tangu ligi ianze na mechi nyingine tano ikitoka sare.
Bao la kwanza la City lilifungwa dakika ya 20 kipindi cha pili na mshambuliaji hatari na chaguo la kwanza la Mwambusi, Paul Nonga anayevalia jezi namba 26 mgongoni, huku bao la pili likifungwa na Peter Mapunda.
Kocha msaidizi wa Mbeya City, Maka Mwalwisyi ameuambia mtandao wa MATUKIO DUNIANI kuwa mchezo ulikuwa mgumu sana kwao, lakini waliingia kupambana na kutafuta ushindi.
“Mechi ilikuwa ngumu sana, lakini kila mara tunasema kuwa tunatafuta pointi tatu na leo hii tunamshukuru Mungu kwa kupata matokeo haya. Tutaendelea kujipanga zaidi, cha msingi mashabiki wa Mbeya wawe na subiri kwani mambo yanakwenda vizuri”. Alisema Maka.
JKT Oljoro lep wameonja joto la jiwe baada ya kula nakozi ya mabao 2-1 nyumbani kwao kutoka kwa Mbeya City
Katika dimba la CCM Mkwakwani jijini Tanga, wagosi wa Kaya, Coastal Union waliwakaribisha wana Lambalamba Azam fc kutoka jijini Dar es salaam na matokeo ya dakika tisini ni suluhu ya bila kufungana.
Nao JKT Ruvu walikabiliana Kagera Sugar katika uwanja wa Azam Complex na kushuhudia dakika tisini zikimalizika kwa wapiga kwata kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.
Kocha msaidizi wa JKT Ruvu fc, Greyson Haule alisema mchezo ulikuwa mzuri na timu zote zilikuwa zinashambuliana, lakini wao walikuwa makini na kutumia nafasi hizo mbili kati ya nyingi walizopoteza.
“Kagera Sugar ni timu nzuri, imecheza vizuri, lakini sisi ni wazuri zaidi na ndio maana tumepata ushindi”. Alisema Haule.
0 comments:
Post a Comment