Wednesday, October 23, 2013


KIIZA GOAL 
Huyu jamaa ni noma!: Diego wa Kampala ambaye jina la kupewa na wazazi wake ni Khamis Kiiza anazidi kuwa lulu kwa kupachika mabao, leo kapiga zake mbili sasa anapumzika tu.
……………………………………………………………………………………………………………
Na Baraka Mpenja , Dar es salaam
LIGI kuu soka Tanzania bara imeendelea kushika kasi  leo hii kwa mechi tatu kupigwa viwanja vitatu tofauti nchini.
Wekundu wa Msimbazi Simba wamepaa tena kileleni licha ya kutoa suluhu ya bila kufunga dhidi ya Coastal Union uwanja wa Mkwakwani Tanga, na kufikisha pointi 20 sawa na Azam fc,na Mbeya City, lakini Mnyama ana wastani mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa ukilinganisha na timu hizo zilizokuwa nafasi mbili za juu.
Kwa maana hiyo, Simba anarejea kileleni na katika nafasi ya pili anabakia Azam fc, huku, Mbeya City wakiwa nafasi ya tatu, huku wakisubiri mechi za wikiendi hii ambapo watapambana na Tanzania Prisons, huku Azam fc akila sahani mojha na Simba.
Kikosi cha Simba SC leo kilikuwa; Abbel Dhaira/Abuu Hashimu dk35, Nassor Masoud ‘Chollo’/Edward Christopher dk67, Haruna Shamte, Gilbert Kaze, Joseph Owino, Jonas Mkude, William Lucian ‘Gallas’, Said Ndemla, Amisi Tambwe, Amri Kiemba/Zahor Pazi dk46 na Ramadhani Singano ‘Messi’.
Coastal; Shaaban Kado, Mbwana Hamisi, Othman Tamim, Marcus Raphael, Juma Nyosso, Jerry Santo, Daniel Lyanga/Uhuru Suleiman dk77, Chris Odula, Yayo Lutimba, Haruna Moshi ‘Boban’ na Kenneth Masumbuko/Pius Kisambalae dk86.
IMG_8254 - Copy 
Shughuli ya Mkwakwani leo: Licha ya Simba kuambulia suluhu, lakini wamepaa kileleni kwa wastani mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa
Jijini Dar es salaam katika dimba la Taifa, wanajangwani Young Africans ambao ndio mabingwa watetezi waliwakaribisha Mafaande wa Jeshi la wananchi Tanzania kutoka mkoani Tabora Rhino Rangers na kushudia Hamis Kiiza akifunga mawili katika dakika ya 12 na 81, huku Frank Domayo naye akifunga dakika ya 73 na kukamilisha ushindi wa mabao 3-0.
Katika mchezo wa leo hadi mapumziko, Yanga walikuwa mbele kwa bao 1-0, na kipindi cha pili kikosi cha Ernie Brandts kilichofanyiwa marekebisho kwa baadhi ya wachezaji kutopangwa akiwemo kipa Ally Muspha Bartez kiliongeza mawili na kuvuna pointi tatu muhimu.
Wachezaji wa Yanga inaonekana walikalishwa na kukalipiwa mno kwani wamecheza soka la uhakika na nidhamu kubwa wakitaka kukwepa makosa waliyoyafanya katika mchezo wa watani wa jadi jumpili ya wiki iliyopita ambao walitoka sare ya 3-3 wakati walimaliza kipindi cha kwanza wakiwa mbele kwa mabao matu.
Simba walisawazisha yote kipindi cha pili na sababu kubwa ilikuwa ni kujiamini kwa wachezaji wa Yanga hasa kipindi cha kwanza kwani walionesha mbwembwe nyingi bila kujua kuwa soka ni dakika 90.
Kikosi cha Yanga SC: Deo Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, David Luhende/Oscar Joshua, Mbuyu Twite, Kevin Yondan, Rajab Zahir, Simon Msuva/Nizar Khalfan dk60, Frank Domayo, Hamisi Kiiza, Mrisho Ngassa na Haruna Niyonzima.
Kikosi cha Rhino Rangers: Mahmoud Othman, Ally Mwanyiro, Hussein Abdallah, Julius Masoga, Ladislaus Mbogo, Stanslaus Mwakitosi, Shijja Mongo, Imani Noel/Msafiri Hamisi dk52, Victor Hangaya/Kamana Salum dk60, Saad Kipanga na Nurdin Bakari. 
Mbali na mechi hizi mbili zilizowakutanisha wakongwe wa soka la Tanzania, mechi nyingine ilikuwa kule jijini Mbeya katika uwanja wa Sokoine ambapo wenyeji Tanzania Prisons walishuka dimbani kuwakabili wakata miwa wa Kaitaba, Kagera Sugar.
Matokeo ya mchezo huo ni sare ya 1-1, na Prisons wanazidi kuchanganyikiwa zaidi kwani wamekuwa wakifanya vibaya sana msimu huu.
Kibaya zaidi wikiendi wanakabiliwa na mechi ngumu dhidi ya watani wao Mbeya City ambao wamekuwa wakifanya vizuri na mpaka sasa hawajapoteza mchezo hata mmoja na wapo nafasi za juu wakijikusanyia pointi 20 sawa na Azam fc pamoja na vinara Simba sc.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video