Sheikh
Issa Ponda akishuka kwenye basi la Magereza tayari Kuingia Mahakama ya
Hakimu Mkazi Mkoani Morogoro leo ambapo Mahakama Ilikuwa inatoa Maamuzi
kuhusu Kufutiwa shitaka moja kati ya matatu yanayomkabili Sheikh Ponda.
Mahakama
Imetupilia Mbali Ombi hilo na kesi itaendelea Kusikilizwa katika
Mahamama hiyo. Kesi hiyo imeahiriswa Mpaka tarehe 7 November mwaka huu
ambapo mahakama itaanza kusikiliza Mashahidi wa kesi hiyo.Sheikh Ponda
Amerudiswa Rumande.
Sheikh Issa Ponda akiingia katika viwanja vya mahakama ya Hakimu mkazi mkoa wa morogoro..
Sheikh Ponda akiwa mahakamani akimsubiri Hakimu tayari kusikiliza Kesi yake katika Mahakama ya Hakimu mkazi Mkoa wa morogoro
Mke wa sheikh Ponda akiwa mahakamani
Ulinzi ukiwa umeimarishwa mahakamani leo wakati kesi hiyo ikiendelea katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa wsa morogoro
PICHA NA MATUKIO NA MICHAPO BLOG
0 comments:
Post a Comment