Mshehereshaji
wa Mjadala wa wazi ulioandaliwa na Umoja wa Mataifa wenye kauli mbiu
“The Future We Want” katika kuadhimisha wiki ya Umoja wa mataifa
kusheherekea miaka 68 ya kuanzishwa kwa Umoja huo akiwatambulisha
Wachokonozi wa Mada Meza kuu Mh Janeth Mbene, Naibu waziri wa Fedha (wa
pili kushoto) Bi. Dorothy Usili, Mwakilishi Msaidizi wa UNFPA ( wa pili
kulia), Paul Mashauri Mwenyekiti wa East Africa Speakers Bureau ( wa
kwanza kulia) na Dakta. Lwidiko Mhamilawa, Mwenyekiti wa Asasi ya Vijana
wa Umoja wa Mataifa (YUNA).
.Ajira kwa vijana si bomu kama watapata mafunzo ya ujasirimali na mitaji
.Serikali yaahidi kuendelea kusaidia vijana kwa maslahi mapana ya taifa
Na Moblog Team
SERIKALI
imewataka vijana kuachana na fikra potovu za kuajiriwa pindi
wanapomaliza masomo yao na badala yake wafikiri zaidi kujiajiri ili
kuweza kupambana na kuondoa kabisa tatizo la ajira nchi. Moblog
inaripoti.
Kwa
muda mrefu watu wa kada mbalimbali wasomi, viongozi wa dini na wanasiasa
wameonya kwamba tatizo la ajira kwa vijana nchini ni bomu linalosubiri
kulipuka wakati wowote kutokana na ukweli kwamba fursa za ajira zimekuwa
chache nchini.
Akizungumza
kwenye Mjadala wa Wazi katika kusheherekea Maadhimisho ya wiki ya Umoja
wa mataifa jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Janet
Mbene amesema asilimia 75 ya watu hapa nchini ni vijana chini ya umri
wa miaka 35 ambayo ndiyo nguvu kazi ya taifa.
Pichani
juu na chini ni Naibu Waziri wa Fedha Bi. Janeth Mbene akitoa mada yake
juu ya mstakabali wa Vijana katika kupambana na tatizo la Ajira nchini
na nafasi ya Serikali katika kuwasaidia vijana kujikwamua kutoka katika
lindi la umaskini.
‘Ni
muhimu kwa vijana nchini kutambua kwamba kwa wingi wao wanaweza
kubadilisha mwelekeo wa nchi na mustakabali wa maisha yao kwa ujumla kwa
kutambua kwamba wao wana fursa adhimu ya kufanya mabadiliko kwa maslahi
mapana ya taifa,’ amesema
“Vijana
wa Tanzania lazima waanze kuchangamkia fursa za mikopo mbalimbali
iliyotegwa na Serikali kupitia Wizara ya Kazi, Ajira na Vijana kwa
sababu kwa sasa Serikali si mwajiri mkubwa kama zamani,” alisisitiza
Amesema
kuwa vijana wameacha fursa kadhaa za kujifunza na kupitia malengo na
mikakati kadhaa ya Serikali kwa sababu ya kutokupenda kujisomea na
kufuatilia sera na mipango mbalimbali ya vijana inayotolewa na Serikali.
Mbene
amesema Wizara ya Fedha kupitia benki kuu ya taifa inayo programu ya
kuwawezesha vijana kiuchumi kwa kuwapa mikopo ya ujasirimali ili waweze
kujiajiri na kuondokana na tatizo la ajira.
Amesema
Serikali itaendelea kutengeneza mazingira mazuri kwa vijana kujiajiri
kwa kuwapatia mikopo, stadi za maisha na mafunzo ya ujasirimali ili
waweze kuwa wabunifu katika biashara zao na kusukuma mbele gurudumu la
maendeleo.
Mwenyekiti
wa East Africa Speakers Bureau Bw. Paul Mashauri akiwaslisha mada yake
juu ya Ujasiriamali na stadi za maisha kwa vijana ambapo pia
amewasisitiza umuhimu wa Vijana wa kutokukata tamaa kwenye biashara.
Kwa
Upande wake Dakta ,Lwidiko Mhamilawa, Mwenyekiti wa Asasi ya Vijana wa
Umoja wa Mataifa (YUNA) amesema vijana kutokana na wingi wao wana kila
sababu ya kuunganisha nguvu zao na kupaza sauti kwa maslahi ya vizazi
vya sasa na vijavyo.
Amesema
kwa muda mrefu vijana wamekuwa nyuma katika kufuatilia mipango ya
Serikali kuhusu vijana na hata sera mbalimbali zinazotungwa bungeni kwa
ajili ya kundi hili vijana wengi hawazijui.
“lazima
vijana wakae chini na wajue wanataka kwenda wapi na wako wapi na nini
changamoto zao kwa sasa katika nchi yao ili waweze kuchangia mijadala
mbalimbali yenye maslahi mapana ya nchi na wao kwa ujumla.
Dakta
Mhamilawa amesema ni fursa pekee kwa vijana kupata wasaa wa kushiriki
katika mijadala mbalimbali ya umoja wa mataifa yenye kuleta hamasa ya
kujifunza kwa bidii stadi mbalimbali za maisha.
Baadhi
ya Wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam wakifuatilia mada
mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa wakati wa maadhimisho hayo.
Mwakilishi
Msaidizi wa UNFPA Bi. Dorothy Usili akiwasilisha mada chokonozi ya
umuhimu wa Vijana kujitambua katika kujiletea maendeleo.
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakiwamo raia wa kigeni wakifuatilia mada hizo.
Dakta.
Lwidiko Mhamilawa, Mwenyekiti wa Asasi ya Vijana wa Umoja wa Mataifa
(YUNA) akiwasilisha mada yake ya umuhimu wa Vijana kujijengea tabia ya
kujisomea na kufuatilia sera, mipango na mikakati mbalimbali ya Serikali
itolewayo kwa Vijana.
Pichani
Juu na Chini ni baadhi ya Wanafunzi wa vitivo tofauti chuo kikuu cha
Dar es Salaam wakiuliza maswali wa wachokonozi wa mada.
Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Usia Nkhoma Ledama.
Afisa
Mshiriki wa UN Cares Beatrice Mkiramweni akizungumza na waandishi wa
habari juu ya umuhimu wa kutoa mafunzo ya maabukizi ya Virusi vya Ukimwi
na unyanyapaa.
Afisa
Mtaalamu wa Kitaifa wa UNAIDS Bw. Emmanuel Mziray akizungumzia madhara
ya unyanyapaa yanavyoweza kuchangia maambukizi mapya ya Virusi vya
Ukimwi kwenye sehemu za kazi na maeneo mbalimbali wakati wa mjadala wa
wazi kwa Vijana katika kusheherekea wiki ya Umoja wa Mataifa nchini
uliofanyika kwenye Ukumbi wa Nkurumah Chuo Kikuu cha Dar es Saalaam.
Baadhi
ya wafanyakazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa wakibadilishana mawazo
na baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuhusiana na
matumizi sahihi ya Condom.
Baadhi
ya wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa nje ya ukumbi wa Nkurumah Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam palipofanyika mjadala wa wazi jijini Dar.
0 comments:
Post a Comment