Sunday, October 6, 2013

wama5Na Anna Nkinda – Maelezo
Serikali ya Japani kupitia Ubalozi wake nchini imetia saini mkataba na  shule ya Sekondari ya wasichana ya WAMA-Nakayama iliyopo Rufiki mkoani Pwani kwa ajili ya msaada wa vifaa vya maabara,  ujenzi wa  zahanati na kutoa mtambo wa maji wa kutumia genereta utakaogharibu Shilingi milioni mia moja na sabini.
Utiwaji saini wa makubaliano hayo ulifanyika jana katika shule hiyo ambayo ni ya watoto yatima, maskini  na wanaoishi katika mazingira magumu kati ya balozi wa Japani Nchini  Masaki Odaka na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) na kushuhudiwa na wageni mbalimbali akiwemo Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete aliyekuwa katika ziara ya kikazi wilayani Rufiji.
Akiongea mara baada ya utiwaji saini wa makubaliano hayo Rais Dk. Kikwete aliwataka wanafunzi hao kusoma kwa bidii kwani wametoka katika mazingira magumu, maskini  na wengine ni yatima elimu peke yake ndiyo itakayowakomboa kimaisha na kuwapeleka katika mazingira mazuri.
Rais Dk. Kikwete pia alimpongeza  Mke wake Mama Salma Kikwete  kwa kufikiria kuwa na wazo la kuanzisha   shule kama hiyo ambayo leo hii imewapa nafasi ya kusoma katika mazingira mazuri watoto wa kike wanaotoka  katika mazingira magumu na kuwataka kutumia  nafasi hiyo  kusoma kwa bidii kwani walimu walio nao ni wazuri na mazingira ya shule ni mazuri.
“Sisi wazee wenu tupo, tutaendelea kuwasaidia na kuwaunga mkono ili mpate mafanikio, hakuna kingine tutakachoweza kuwaombea zaidi ya hili, mmetoka katika mazingira  magumu wengine ni yatima elimu ndio itakayowatoa katika mazingira hayo na kuwafikisha katika mazingira mazuri,” alisema Rais Dk. Kikwete.
Rais Dk. Kikwete pia aliwapongeza wanafunzi hao kwa kufanya vizuri katika mitihani yao ya kidato cha pili na kushika nafasi ya kwanza kiwilaya na kuwataka  kufanya vizuri zaidi  ili waweze kuongoza hadi ngazi ya  taifa.
Kwa upande wake Balozi Odaka alisema wazo la mradi huo wa kuboresha mazingira ya kusomea kwa wanafunzi ulianza miaka kadhaa iliyopita baada ya uzinduzi wa shule hiyo na Taasisi ya Nakayama ya nchini Japani.
Alisema mradi huo unasura tatu ambazo ni kutoa vifaa vya maabara, kutayarisha zahanati yenye vifaa na kutoa mtambo wa maji ya kutumia genereta karibu na zahanati na mabweni. Msaada huo utaboresha mazingira ya kusomea kwa wanafunzi, kufanya kazi kwa wafanyakazi wote wa shule hiyo pamoja na shule jirani ya Sekondari ya Nyamisati.
“Pamoja na mradi huu kama kuna mahitaji mengine zaidi ya kuboresha mazingira ya kusomea shuleni hapa, Serikali ya Japani ingependa kuzingatia ili kuridhisha mahitaji ya wanafunzi kwani tunapenda kuendeleza misaada ya mahitaji muhimu ya kibinadamu nchini Tanzania”, alisema Balozi Odaka.
Aidha Balozi huyo pia alimpongeza mama Kikwete  kwa mchango wake wa maendeleo ya wanawake nchini na kusema kuwa shule hiyo na mradi huo usingekuwepo bila ya jitihada zake.
Naye Mama Kikwete aliwashukuru watu wa Japani kwa msaada muhimu wa maendeleo ya kitaaluma utakaosaidia kuboresha ufundishaji wa majaribio ya masomo ya sayansi na huduma ya afya kwa wanafunzi na Jumuiya  ya WAMA-Nakayama .
Mwenyekiti huyo wa WAMA alisema lengo kuu la shule hiyo ni kutoa elimu bora ya Sekondari kwa watoto wa kike waliotoka katika mazingira hatarishi na yatima kwani elimu ni nyenzo muhimu ya kumuwezesha mtu kujikwamua kutoka katika hali ya umaskini, ujinga na maradhi.
“Elimu ya Sekondari kwa mtoto wa kike inamuwezesha kuepuka mimba za utotoni , vifo vinavyotokana na uzazi kwani asilimia 20 ya vifo vya kina mama vinatokana na uzazi katika umri mdogo. Pia elimu itawasaidia  kufaidika na fursa mbalimbali za elimu ya juu na kujiendeleza kiuchumi”, alisema Mama Kikwete.
Alisema wamejenga maabara nne ambazo zitawezesha ufundishaji wa masomo ya sayansi na kupatikana kwa vifaa hivyo kutawasaidia wanafunzi kutekeleza mafunzo kwa vitendo kwa kiwango cha juu na hivyo kuongeza ufaulu katika mitihani yao.
Akisoma taarifa ya shule Kaimu Mkuu wa Shule Mwalimu Suma Mensah alisema shule hiyo  ni kipekee kwani inachukua wanafunzi kutoka Tanzania nzima ambao wanatoka familia duni, mazingira magumu na yatima.Shule inawasaidia kwa  asilimia mia moja kwa kuwapatia chakula,malazi na mavazi, kuwapatia  nauli wanaporudi nyumbani wakati wa  likizo na wanaporudi shule na pesa kidogo za matumizi wanapokuwa safarini.
Mwalimu  Mensah alisema wamekuwa na mikakati kadhaa ya kuboresha taaluma ikiwa ni pamoja na kuongeza muda wa ziada wa kufundisha na kuwasaidia wanafunzi. Lengo kubwa ni kumaliza sillabasi mapema na kuanza kufanya marudio ili wanafunzi waweze kuelewa zaidi na kuandaa mitihani mingi ya ndani na nje ya shule hii ikiwa ni maandalizi ya mitihani mbalimbali ya kitaifa.
 “Tunamshukuru Mama yetu mpendwa Salma Kikwete kwa kutuletea Mtaalamu wa kompyuta ili aweze kutufundisha.Tunaamini baada ya  kumalizika kwa kozi hii,walimu tutakuwa na uwezo wa kuandaa masomo yetu kwa kutumia kompyuta na kufundisha kwa njia ya kisasa yaani ‘projector’ madarasani”, alisema.
Shule ya WAMA-Nakayama  iko chini ya Taasisi ya WAMA ilianzishwa mwaka 2010 ikiwa na wanafunzi 82, walimu watano na wafanyakazi wasio walimu watano ilizinduliwa  mwaka 2011.Hivi sasa shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 322 wa kidato cha kwanza mpaka cha nne na wafanyakazi ishirini na saba 27,walimu16 na wafanyakazi wasio walimu 11.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video