Friday, October 4, 2013

44Mahmoud Ahmad Arusha
Serikali imesema kuwa itapambana na wale wote wanaouwa wanayamapori wakiwemo Tembo kwani imeonekana jamii ya tembo hapa nchini imepungua kwa kasi kutokana na ujangili wa meno ya tembo unaotikisa mataifa kadhaa ya Afrika.
Kauli hiyo imetolewa leo kwenye matembezi ya kupinga ujangili wa Tembo yaliofanyika kwenye viwanja vya Aicc Kijenge na mgeni rasmi alikuwa ni Waziri wa maliasili na utalii Balozi Khamis Kagasheki.
Akizungumza kwenye Hafla hiyo Balozi Kagasheki alisema serekali imeshaanza kupambana na majangili wanauwa wanyamapori akiwemo Tembo kwani kwa sasa operesheni hiyo itaongozwa na Jeshi la wananchi na kuwa siku zao zinahesabika.
“Operesheni uhai namba mbili imeshaanza kutokana na kauli ya raisi jakaya Kikwete aliyotoa kuwa hatakubali kuona akilaumiwa kutokana na vitendo ya ujangili kwani yeye raisi hatakubali kuopna maliasili na wanyamapori wakitokweka mikononi mwake”alimnukuu Rais
Waziri Kagasheki akawataka Watanzania kupambana kwa nguvu na kushirikiana na serekali yao katika vita hiyo ya ujangili na kuwa sheria zimekuwa zikizidi kuwaweka katika wakati mgumi kwani mtu anauwa wanyamapori halafu analipa faini unategemea ujangili utakwisha kwa mtindo huu.
Aidha alisema kuwa anatarajia kupeleka kwenye bunge muswada wa sheria kubadili hukumu wanayopata majangili wa wanyamapori kwani adhbu wanazopata zimekuwa kiduchu kulingana na makosa yao huku akiwalamu watetezi wa haki za binadamu kutetea majangili hao wa meno ya tembo.
Unajua hapa kuwa majangili sisi sote tunawajua wanapirta kwenye maeneo yetu wakitumia nyumba zetu vijiji vyetu sasa tushirikiane kuwafichua ilikukomesha ujngali hapa nchini.
Akizungumza wakati akimkaribisha waziri mkuu wa mkoa wa Arusha Magesa Mulongo alisema Majangili wapo kwenye kaya zetu nyumba zetu hivyo vita hii si ya serekali pekee kwani itakuwa aibu kubwa kwa vizazi vijavyo kuja kuona historia ya mnyama Tembo wakati tunaweza kumbakisha akiwa salama na kuja wakabidhi watoto wetu kama urithi.
Mulongo alisema kuwa anasikitika kuona idadi iliyoongezeka ikishuka kwa muda mfupi huku watanzania wakiwa kimya bila ya kutoa kelele lakini leo nimefarijika kuona watanzania wenzangu wamekumbuka wajuibu wao kwa kutangaza vita vya jangili kwa vitendo ikiwemo matembezi haya.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video