Semina ya mafunzo ya siku nne kwa watendaji na viongozi wa CCM ngazi za
wilaya na mikoa nchini kote, ambavyo ilianza jana mjini Dodoma kwa
kufunguliwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Zanzibar, Dk. Ali
Mohamed Shein, leo imeendelea kupamba moto kwa mada mbalimbali, katika
ukumbi wa sekreterieti ndani ya Jumba la White House, Makao Makuu ya CCM
mjini Dodoma.
Pichani,
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akitoa maneno ya utangulizi
kabla ya mada kuanza kutolewa. Wengine kutoka kushoto ni Naibu Katibu
Mkuu wa CCM (Bara) Mwigulu Nchemba, Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha,
Zakiah Meghji na Katibu wa NEC, Itukadi na Uenezi Nape Nnauye.

Nape akitoa angalizo kuboresha usikivu wa mada kwenye semina hiyo
Imetayarishwa na theNkoromo Blog
0 comments:
Post a Comment