
MPAMBANO wa masumbwi uliokuwa
ukutanishe kati ya Bondia Kalama Nyilawila na Sado Philemon uliokuwa
uchezwe Oktoba 20 jumapili katika uwanja wa CCM Mwijuma Mwananyamala
umeahirishwa kutokana na kupisha mpambano wa watani wa jadi Simba na
Yanga utakaofanyika katika uwanja wa taifa
Akizungumza mratibu wa mpambano huo Ibrahim Kamwe ‘amesema
mpambano huo umeahirihwa kwa muda kupisha mchezo wa Simba na Yanga kwa
kuwa mashabiki wa mpira ndio hao hao mashabiki wa mchezo wa masumbwi
hivyo kwa sasa mpambano huo utafanyika Novemba 3 katika ukumbi uho huo.Mwaite Juma na Shadrack Ignas , nae bingwa wa zamani wa Bantam Ajibu Salum atapimana ubavu na Martin Richard,huku Mbena Rajab akizipiga na Godwin Mawe, Ibrahim Class ‘King Class Mawe ‘ atazichapa na Rashid Ali, Hassan Kiwale (Moro Best) na Harman Richrd, Kasim Chuma na Shaban Manjoly, mdogo wake Francis Miyeyusho Yona miyeyusho atacheza na julias Thomas, Abdalla ruwanje na Bakari Zoro, na kutakuwepo na pambano la kitaa kwa mbabe wa Mwananyamala sokoni Joseph Stanslaus(Amita au Jose Mawe) na mbabe wa Manzese sokoni Shaban Seif(Body Kitongoji) pambano linalotarajiwa kuwa na vituko kwa mabondia hao, Nae Yasin Omari atazichapa na Innocent Gabriel pamoja na mapambano mengine kadhaa ya vijana wadogo wenye vipaji vya mchezo wa ngumi.
Mapambano haya yote yameandaliwa
na Ibrahim Kamwe wa Bigright Promotion kwa kusindikiza pambano la ISSA
OMAR(Peche Boy) atakaezipiga na ATHONY MATHIAS katika pambano la ound
nane na SADO PHILEMON atazipiga na KARAMA NYILAWILA katika uzito wa
middle kutafuta mshindi wa atayepigana na Thomas Mashali katika pambano
la ubingwa.
Kwa ufupi mabondia wote wapo
katika hali nzuri na wametakiwa kuendelea na mazoezi kwa ajili ya
mapambano hayo yatakaofanyika mwanzoni mwa mwezi ujao katika ukumbi wa
CCM Mwinjuma Mwananyamala A
0 comments:
Post a Comment