Rais
mpya wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, Jamal Malinzi ameendelea
kupokea salamu za pongezi baada ya kushinda wadhifa huo katika uchaguzi
uliofanyika Oktoba 27 mwaka huu.
Salamu
nyingine za zimetoka kwa Rais wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa
Miguu (FIFA), Sepp Blatter ambapo amempongeza Malinzi kwa kuchaguliwa na
kumtakia kila la kheri katika majukumu yake ya kuongoza mchezo huo
nchini.
Blatter
amesema ana uhakika ufahamu wake na uwezo wake katika uongozi ni muhimu
katika kuimarisha maendeleo ya mpira wa miguu nchini, na kuongeza kuwa
milango ya FIFA iko wazi wakati wowote anapotaka kujadili masuala
yanayohusu mchezo huo.
“Nakutakia
wewe na kamati mpya ya Utendaji iliyochaguliwa kila la kheri, nguvu, na
kila aina ya mafanikio kwa changamoto zilizo mbele yenu,” amesema Rais
Blatter katika salamu zake.
Wengine
waliomtumia Rais Malinzi salamu za pongezi ni Rais wa Shirikisho la
Mpira wa Miguu la Kenya (FKF), Sam Nyamweya, Rais wa Heshima wa
Shirikisho la Vyama vya Mpira wa Miguu Uganda (FUFA), Lawrence Mulindwa,
Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mwanza (MZFA) na Mwenyekiti wa Chama
cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Arumeru (ADFA), Peter Temu.
YANGA, JKT RUVU UWANJANI KESHO
Raundi
ya 12 ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inaendelea kesho (Novemba 1 mwaka
huu) kwa mechi kati ya JKT Ruvu na Yanga itakayochezwa Uwanja wa Taifa,
Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni.
Viingilio
katika mechi hiyo ni sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 kwa
VIP A. Tiketi zitauzwa siku ya mechi uwanjani katika magari maalumu
kuanzia saa 4 asubuhi.
Novemba
2 mwaka huu kutakuwa na mechi nne; Mgambo Shooting na Coastal Union
(Uwanja wa Mkwakwani, Tanga), Tanzania Prisons na Oljoro JKT (Uwanja wa
Sokoine, Mbeya), Azam na Ruvu Shooting (Azam Complex, Dar es Salaam), na
Mtibwa Sugar na Rhino Rangers (Uwanja wa Manungu, Morogoro).
Raundi
hiyo itakamilika Novemba 3 mwaka huu kwa mechi moja ambapo Mbeya City
itakuwa mwenyeji wa Ashanti United kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya
Sokoine jijini Mbeya.
Mechi
za kukamilisha mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo zitachezwa Novemba 6 na 7
mwaka huu. Novemba 6 ni JKT Ruvu vs Coastal Union, Ashani United vs
Simba, Kagera Sugar vs Mgambo Shooting, Rhino Rangers vs Tanzania
Prisons na Ruvu Shooting vs Mtibwa Sugar.
Novemba 7 mwaka huu, Azam itacheza na Mbeya City wakati Yanga itacheza na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment