WASHAMBULIAJI
Neymar na Robinho walionekana kutaka sana kubadilishana jezi katika
mechi baina ya timu zao, AC Milan na Barcelona Ligi ya Mabingwa jana
usiku… na wakafanya hivyo wakati wa mapumziko!
Licha
ya kuchezea wote timu ya taifa ya Brazil, Robinho anabakia kuwa shujaa
mkubwa wa Neymar na wawili hao walibadilishana jezi wakati refa
anamaliza kipindi cha kwanza.
Neymar
alitoa heshima zake kwa winga wa Milan, anayemzidi miaka nane, kabla ya
mchezo wa jana, lakini akamuonyesha kazi uwanjani.
Neymar
aliposti picha yake akiwa mdogo pamoja na nyota huyo wa zamani wa Man
City katika Instagram akisema: “Leo ni siku maalum kwangu…kwa kucheza
kwa mara ya kwanza dhidi ya mkali wangu, ambaye nimekuwa nikimfuatilia
wakati wote tangu nikiwa mdogo na ni heshima kucheza dhidi yake. Bahati
nzuri wakati wote, lakini leo ni Barca hahahah, nakupenda,”.
Wachezaji wote walianzia soka yao klabu ya Santos ya Brazil kabla ya kuhamia Ulaya kwa uhamisho wa fedha nyingi.
Robinho
alihamia Real Madrid mwaka 2005, akisajiliwa na vigogo hao wa Hispania
kwa dau la Pauni Milioni 20 wakati Neymar alitua Barcelona mapema msimu
huu kwa pauni Miloni 50.
Miaka hiyo: Neymar ameposti picha yake akiwa na shujaa wake Robinho kwenye Instagram jana
Pozi: Robinho akizungumza na Neymar baada ya mechi ya AC Milan na Barcelona Uwanja wa San Siro
Wakati huo huo, mechi hiyo ya Kundi H iliisha kwa sare ya 1-1. Bahati mbaya kwa Neymar, alimshuhudia Robinho akiwafungia bao la kuongoza The Rossoneri dakika ya 10, baada ya mabaki wa Barca kujichanganya.
Javier
Mascherano alichanganyana na beki mwenzake Gerard Pique na Robinho
akaunasa mpira kabla ya kugongeana pasi na Mbrazil mwenzake Kaka, kisha akafunga.
Pamoja na hayo, bao la Milan halikudumu sana baada ya Lionel Messi kusawazisha dakika 13 baadaye.
Bao la kuongoza: Robinho alitumia mwanya wa mabeki wa Barcelona kujichanganya kuifungia Milan bao la kuongoza
Mfungaji wa bao: Robinho akishangilia baada ya kuifungia The Rossoneri jana
La kusawazisha: Lionel Messi akimfunga kipa Marco Amelia kuisawazishia Barcelona
Umalizijia mzuri: Messi akipongezwa na wenzake, Wabrazil Dani Alves na Neymar baada ya kufunga
0 comments:
Post a Comment