Saturday, October 19, 2013

CIMG2721 
Na Gladness Mushi  Arusha.
Jeshi la zima moto na ukoaji mkoa wa Arusha linakabiliwa na changamoto ya uchakavu wa nyumba uliodumu kwa miaka zaidi ya 50 ambapo pia
uchakavu huo wa nyumba unaenda sanjari na uhaba wa Vyoo hali ambayo inasababisha ongezeko la magonjwa ya Malaria kutokana na nyumba hizo kugeuka kuwa makazi ya Mbu.
Aidha nyumba hizo zilijengwa mwaka 1954 ambapo mpaka sasa hazijaweza kufanyiwa marekebisho ya aina yoyote ile hali ambayo inasababisha
nyumba hizo kugeuka magofu.
Hayo yamelezwa na Andrew James Mbate ambaye ni kamanda Zima moto na uokoaji mkoa wa Arusha wakati akiongea na wafanyakazi wa jeshi hilo
mara baada ya kumuaga aliyekuwa kamanda wa jeshi hilo Bw Jesward Ikonko mapema jana.
Kamanda Andrew alisema kuwa nyumba hizo za jeshi zilijengwa miaka mingi iliyopita lakini toka kujengwa kwake mwaka 1954 mpaka sasa hazijaweza kufanyiwa marekebisho ya aina yoyote ile jambo ambalo linasababisha wafanyakazi pamoja na familia zao ziweze kuishi maisha ya kuugua kila mara.
“Tunaweza kusema kuwa nyumba hizi zimegeuka nyumba za mbu kwani kwa juu hazijaweza kuzibwa na baridi yote inapita lakini pia hata kwa juu kwa kuwa kuna uwazi mkubwa sana unasababisha mbu kukaa kama nyumbani kwani sasa hali hiii kwa kweli inasababisha wafanyakazi wetu washindwe kufanya kazi zao kwa kufuraia makazi’aliongeza hivyo.
Pia alisema kuwa mbali na nyumba hizo kugeuka chakavu sana lakini pia hata suala la vyoo navyo ni chakavu kwa kiwango cha hali ya juu jambo
ambalo ni hatari kwa afya za watumiaji
“tunaweza kujiuliza kuwa choo kilichojengwa mwaka 1954 mpaka sasa kitakuwaje na kinatumiwa na familia nyingi je kwa hali hii wafanyakazi wataweza kufuraia maisha au ndo wataboreka “alihoji Kamanda huyo.
Kutokana na hali hiyo alisema kuwa ni vema kama mchakati wa nyumba hizo za watumishi sasa zikageukia upande wa Wizara kutoka katika
mikono ya Jiji la Arusha kwani kama zitakuwa chini ya wizara zitaweza kupata marekebisho makubwa ambayo yataongeza utendaji kazi mzuri wa wafanyakazi.
Akiongelea suala zima la utendaji kazi wa kikosi hicho cha zima moto mkoa wa Arusha alisema kuwa mkoa wa Arusha unakabiliwa na tatizo la
ujenzi holela hali ambayo inasababisha wakati mwingine washindwe kuokoa baadhi ya nyumba ambazo zinateketea kwa Moto hivyo basi ni vema kama kamati ya mipango miji wakati mwingine ikawa inatoa elimu kwa wananchi wanaotaka kujenga nyumba zao.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video