SACP, James Kombe enzi za uhai wake |
Mwili
wa aliyekuwa Kamanda Mstaafu wa Kikosi cha Usalama Barabarani
Kamishina Msaidizi Mwandamizi (SACP), James Kombe utaagwa Ijumaa katika
Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania lililopo Usharika wa Msasani
jijini Dar es salaam.
Hayo
yalisemwa na Mwenyekiti wa kamati ya mazishi inayojumuisha Familia ya
marehemu na Jeshi la Polisi, Naibu Kamishi wa Polisi (DCP) Thobias
Andengenye.
Aliongeza
kuwa ndugu, jamaa, marafiki maofisa wa polisi, askari pamoja na
viongozi mbalimbali watapata fursa ya kutoa heshima za mwisho kwa mwili
wa Marehemu na baadae mwili utasafirishwa kuelekea Moshi, mkoani
Kilimanjaro kwa ajili ya mazishi.
James Kombe alifariki dunia Oktoba 22 mwaka huu wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Ocean Road jijini Dar es Salaam.
Kombe
alizaliwa mwaka 1950 huko Mwika mkoani Kilimanjaro na alijiunga na
Jeshi la Polisi tarehe 15 mwezi machi mwaka 1970 baada ya kuhitimu elimu
ya sekondari mwaka 1969 nchini Uganda ambapo alipandishwa vyeo na
kupewa madaraka mbalimbali.
0 comments:
Post a Comment