Tuesday, October 15, 2013

Kutoka kushoto (mstari wa mbele) ni Waziri wa Utumishi Mh.Celina Kombani,Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk.Rehema Nchimbi,Mstahiki Meya wa Manispaa ya Dodoma Mh.Emmanuel Mwiliko na Naibu Katibu Mkuu Utumishi Bw.HAB Mkwizu wakiserebuka katika maadhimisho ya siku ya Baba wa Taifa katika viwanja vya Nyerere Square mjini Dodoma.Wengine vi viongozi waandamizi serikalini walioalikwa kwenye maadhimisho hayo. SONY DSCWaziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mh.Celina Kombani akihutubia wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mwalimu Nyerere katika viwanja vya Nyerere Square mjini Dodoma. SONY DSCKikundi cha Ngoma za Asili cha ‘Hiyari ya Moyo’ kikitoa burudani katika Maadhimisho ya Siku ya Kumuenzi Baba wa Taifa katika viwanja vya Nyerere Square mjini Dodoma. SONY DSCBaadhi ya wakazi wa Mkoa wa Dodoma wakijumuika pamoja kuadhimisha Siku ya Kumuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere katika viwanja vya Nyerere Square mjini Dodoma. SONY DSCBaadhi ya wakazi wa Mkoa wa Dodoma wakiwemo wananfunzi wakijumuika pamoja kuadhimisha Siku ya Kumuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere katika viwanja vya Nyerere Square mjini Dodoma.
…………………………………………………………………………………………..
Na Happiness Shayo-Utumishi
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere anasifika kwa kujenga misingi ya kizalendo ya umoja wa kitaifa,kufuta ubaguzi wa rangi,dini na kabila,kuweka usawa ,uadilifu na utii wa sheria ambavyo ni nguzo muhimu katika kuleta maendeleo ya taifa.
Hayo yalisemwa mapema leo na Mh.Balozi Job Lusinde katika maadhimisho ya Siku ya Kumuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere yaliyofanyika katika viwanja vya Nyerere Square mjini Dodoma.
Balozi Lusinde aliyekuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo alisema kuwa ili kuhakikisha misingi ya kizalendo inatekelezeka Mwalimu Nyerere alisisitiza falsafa ya ujamaa kwa wananchi iliyohimiza wananchi kuhamia vijijini.
“Mwalimu aliamini kuwa wananchi wote wakihamia vijijini kutakuwa na maendeleo  na ndio maana alitaka watumishi wahamie vijijini”alisema Mh.Lusinde.
Mh.Lusinde alifafanua kuwa Mwalimu Nyerere aliamini kuhamia vijijini kutapelekea mgawanyo wa rasilimali ardhi utakaopelekea kupunguza migogoro ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji.
Aidha,Mh.Lusinde alisema kutotekelezwa kwa falsafa ya ujamaa kumepelekea migogoro ya ardhi inayoonekana sasa.
“Hatukutekeleza falsafa ya ujamaa ndio maana dhambi ya migogoro ya wakulima na wafugaji inaendelea kutumaliza”alisema Mh.Balozi Lusinde.
Naye Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mh.Celina Kombani alisema kuwa ili kuenzi fikra za Mwalimu Nyerere Serikali imetunga sheria ya kuwaenzi Waasisi wa Taifa.
Alisema kuwa serikali imefanikiwa kupata eneo la kujenga kituo cha Kuwaenzi Waasisi wa Taifa ili kuendelea kuenzi mambo mazuri ya Waasisi hao.
“Serikali imepata eneo la kujenga Kituo cha Kuwaenzi Waasisi wa Taifa letu lililopo eneo la Kiromo Bagamoyo”alisema Mh.Kombani.
Aidha,Mh.Kombani alifafanua kuwa pamoja na mambo mengine kituo hicho kitakuwa kinafanya kazi ya kuzikusanya,kuhifadhi kumbukumbu,mali,vitu vyenye umuhimu wa kihistoria vya Waasisi kwa mujibu wa sheria.
Pia,Mh.Kombani alisema ili kuendelea kuwaenzi Waasisi wa Taifa serikali imefanikiwa kuzitambua taasisi na AZAKI zinazomiliki kumbukumbu,mali na vitu vyenye umuhimu kihistoria ili kuhakikisha zinatunzwa vizuri kwa maslahi ya Taifa.
Maadhimisho ya Kumuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mjini Dodoma yameandaliwa na Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma kupitia Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa na yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali na wananchi.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video