Mwenyekiti wa Kituo cha Bravo Job Centre, ambaye pia ni Mbunge wa
Temeke, Abbas Mtemvu akimkabidhi Halima Selemani nyaraka mbalimbali
ikiwemo tiketi ya ndege ya kwenda Dubai kufanya kazi kwa mkataba wa
miaka miwili, katika hafla ya kuwaaga iliyofanyika Dar es Salaam
mwishoni mwa wiki. Kituo hicho kimewatafutia wanawake watano kazi ya
ndani nchini humo. Kutoka kulia ni Asmah Mshangama, Mwajuma Bakari na
Fatma Saburi. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)
Na Richard Mwaikenda
MBUNGE wa Temeke, Abbas Mtemvu
amefanikisha wanawake watano kupata kazi nchini Dubai kwa mkataba wa
miaka miwili na mshahara mnono.
Mtemvu
ambaye ni Mwenyekiti wa Kituo cha Bravo Job chenye ofisi Dubai na Dar
es Salaam, aliwakabidhi tiketi ya kwenda huko pamoja na nyaraka zingine
muhimu ukiwemo mkataba wa kazi.
Waliofanikiwa
kupata fursa hiyo ya kwenda kufanya kazi za ndani ni Halima Selemani,
Fatma Saburi, Asmah Mshangama, Mwajuma Bakari walioondoka jana kwa
ndege ya Qatar pamoja na Nuru Rajab aliyekwenda huko mwezi uliopita.
Akizungumza
wakati wa hafla hiyo ya kuwaanga, Mtemvu aliwataka watanzania hao
kwenda kufanya kazi kwa bidii na nidhamu ya hali ya juu kwa lengo la
kulinda heshima ya Tanzania.
Alisema kuwa endapo kama kuna
mtu atakwenda kinyume,basi yeye na kituo chake wataamua kukatisha
mkataba na kurudishwa haraka nyumbani.
Mtemvu
alisema kuwa moja ya mambo muhimu ambayo inayafanya katika utaratibu wa
kuwatafutia watu kazi nje ya nchi, ni kufuata taratibu zote za
kiserikali za hapa nchini na wanakokwenda kufanya kazi.
Pia
alisema kuwa kituo hicho kina utaratibu wa kwenda kuwatembelea
wafanyakazi hao katika maeneo wanayofanya kazi kwa lengo la kuona kama
wanatendewa vizuri na waajiri wao.
Alitaja
fursa zingine za kazi zinazopatikana katika nchi za Falme za Kiarabu
kuwa ni udereva teksi, ujenzi, upakaji ina na uhasibu na uselemala.
Wanawake hao, waliimpongeza Mtemvu na kituo chake kwa kubuni utaratibu huo na
kuwawezesha kupata kazi, jambo ambalo hawakutarajia katika maisha yao kwamba wanaweza kupata kazi nje ya nchi.Pia waliahidi kutokiuka makubaliano ya mkataba wao.
kuwawezesha kupata kazi, jambo ambalo hawakutarajia katika maisha yao kwamba wanaweza kupata kazi nje ya nchi.Pia waliahidi kutokiuka makubaliano ya mkataba wao.
Kupitia
kituo hicho, Mtemvu ameahidi kuwatafutia kazi watanzania katika nchi za
Falme za Kiarabu na kwingineko duniani, ili kuipunguzia Serikali tatizo
la ajira.
0 comments:
Post a Comment