Wazee wa usafiri wa kukatisha njia kwa haraka maarufu kwa jina la Bodaboda nao wanapaki kivyao tu bila utaratibu maalamu. (Picha na Kibada Wakibada)
…………………………………………………
Na Kibada Wakibaba, Mpanda-Katavi
Halmashauri ya Mji wa Mpanda imeagizwa kuhakikisha inatenga maeneo ya maegesho ya magari ili kuondoa usumbufu uliopo katika mji wa mpanda kwa wenye vyombo vya usafiri kupaki vyombo vyao kiholela hali inayoonesha kuwa hakuna utaratibu unaoeleweka kwa vyombo hivyo kuegeshwa.
Agizo hilo lilitolewa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi Mhandisi Emanuel Kalobelo kufuatia kuwepo kwa maegesho ya magari maeneo yasiyo rasmi hali ambayo inaonesha kuwa ni kukiuka taratibu za mji.
“Wale waliopewa dhamana kusimamia lazima wawajibike kwa hali hiyo nakuagiza mkurugezi kuanzia sasa natoa siku 30 kipindi cha mwezi mmoja kuhakikisha magari yote pikipiki maarufu kama bodaboda zinakuwa na utaratibu mzuri wa maegesho kuliko ilivyo kwa sasa”Alisema Mhandisi Kalobelo Katibu Tawala Mkoa.
Pamoja na maagizo hayo bado mamlaka husika haijatekeleza kama ilivyotakiwa na kila kona ukipita mjini utakutana magari ya Mizigo, Mabasi, pikipiki, na vyombo vingine vya moto vimeegeshwa hovyo katika maeneo yasiyoruhusiwa kana kwamba sheria zimekwenda likizo na maagizo ya viongozi kutotekelezwa na wale wanaopewa majukumu hayo je! Tutafika kwa mtindo huo.
0 comments:
Post a Comment