Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail
KOCHA
wa mabingwa watetezi wa ligi kuu soka nchini England, mashetani
wekundu, Manchester United, David Moyes jana usiku amemfananisha nyota
wake kinda Adnan Januzaj kuwa ni Wayne Rooney mdogo na kusisitiza kuwa
yoso huyo aliyekulia klabuni hapo atasaini mkataba mpya Old Trafford.
Januzaj,
miaka 18, alifunga mabao mawali dhidi ya Sunderland siku chache
zilizopita na sasa yupo katika mashaka ya hatima yake ya baadaye kwani
mkataba wake unamalika mwishoni mwa msimu huu.
Alipoulizwa jana ijumaa kuhusu suala la kijana huyo, Moyes alisema: “Nataka limalizike na klabu ifanye hilo pia. Najiamini”.

Tayari kukaa: Nyota kinda wa Manchester United, Adnan Januzaj anataka kuendelea kukaa klabuni hapo
Januzaj atawakilisha taifa gani?
KOSOVO: Kupitia baba yake, Abedin, ambaye alizaliwa Kosovo. Lakini Kosovo haitambuliwi na FIFA.
BELGIUM: Kupia kulizaliwa huko. Alizaliwa mjini Brussels na ameishi pale mpaka alipojiunga na Manchester.
ALBANIA: Kupitia urithi. Wazazi wake wana asili ya Albanian.
TURKEY: Kupitia familia. Mabibi na mababu zake ni Waturuki.
ENGLAND: Kupitia makazi, kama ataishi miaka mitano ijayo nchini England ataichezea.
BELGIUM: Kupia kulizaliwa huko. Alizaliwa mjini Brussels na ameishi pale mpaka alipojiunga na Manchester.
ALBANIA: Kupitia urithi. Wazazi wake wana asili ya Albanian.
TURKEY: Kupitia familia. Mabibi na mababu zake ni Waturuki.
ENGLAND: Kupitia makazi, kama ataishi miaka mitano ijayo nchini England ataichezea.
‘Una miaka18 na unaichezea Manchester United-Sijui ni wapi unapenda kucheza zaidi”
Bosi
huyo wa Manchester United alimlea Rooney akiwa kijana katika klabu ya
Everton na anaamini Junazaj ana kipaji sawa na nyota huyo.
Moyes alisema: ‘Wayne Rooney, Charlie Nicholas, Paul McStay — Adnan watakuwa katika aina hii ya wachezaji.’
Moyes alikuwa anasikiliza swali juu ya vijana gani wanaomfanya afurahi zaidi Old Trafford na awataje majina yao.
‘Adnan!’ alikuwa kijana wa kwanza kutajwa.

Ana ndoto kubwa: Januzaj anasema anataka kuwa mchezaji bora wa dunia

Kijana mwenye kipaji: Moyes alifanya kazi na Wayne Rooney alikuwa kocha wa Everton

Kiboko cha nyavu: Januzaj aliifungia Man United mawili dhidi ya Sunderland
0 comments:
Post a Comment