Baadhi
ya viongozi wa Mkoa wa Iringa wakiungana na wafanyakazi wa hospitali ya
Rufaaa ya Mkoa wa Iringa wakati wa sherehe ya ufunguzi rasmi wa jengo
la wodi ya watoto lililojengwa kwa ufadhili wa hospitali ya Vicenza
iliyoko katika mkoa wa Veneto huko nchini Italia kwa kushirikiana na
serikali ya Tanzania. Ufunguzi huo ulifanyika tarehe 15.10.2013.
Jengo
la wodi ya watoto lililoko katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa
lililofunguliwa rasmi na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete tarehe
15.10.2013. Jengo hilo la ghorofa moja limegharimu zaidi ya shs 1.8
bilioni na limejengwa kwa ushirikiano wa serikali ya Tanzania na
ufadhili kutoka hospitali ya Vicenza iliyoko nchini Italia.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akifungua rasmi jengo la wodi ya watoto
kwenye hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa kwa kufungua kitambaa huku
akishirikiana na Baba Askofu Tarciusius Ngalalekumtwa wa Kanisa Katoliki
Jimbo la Iringa. Ufunguzi huo ulifanyika tarehe 15.10.2013.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akifungua rasmi jengo la wodi ya watoto
katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa. Hospitali hiyo inahudumia
pia wananchi wa Mkoa wa Njombe. Wengine katika picha hiyo (kulia kwenda
kushoto) ni Baba Askofu Tarciusius Ngalalekumtwa wa Kanisa Katoliki
Jimbo la Iringa akifuatiwa na Balozi wa Italia hapa Tanzania
Mheshimiwa……..,Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dkt. Christine Ishengoma, Mama
Salma, Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali Mama Mofore na wa mwisho ni mmoja
wa wageni waliotoka nchini Italia.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akitembelea chumba cha watoto wanachowekwa
mara tu baada ya mama wa watoto hao kujifungua hospitalini hapo. Katika
picha anaonekana akimhudumia mtoto kwa kumtandikia kitanda chake.
Kulia kwa Mama Salma ni Dkt Clodrick Mwakibopile
Mama
Salma Kikwete akiwaangalia watoto wengine huku akipata taarifa
mbalimbali zinazowahusu watoto hao kutoka kwa Dkt. Mwakibopile wa
hospitali hiyo.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akimsaidia Bi Mwajuma Willy, 17, anayetoka
katika kijiji cha Solanga huko Pawaga, mkoani Iringa kumnyonyesha
mtoto wake aliyejifungua tarehe 11.10.2013 katika hospitali ya Rufaa ya
Mkoa wa Iringa. Mama Salma alitembelea wodi ya watoto mara baada ya
kuifungua rasmi.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akimjulia hali mtoto Saimon Gamaya , mwenye
umri wa miezi 11 na nusu akiwa na Mama yake Vumilia Ernest aliyelazwa
katika jengo la wodi ya watoto akiwa anaumwa sikio na kuharisha. Jengo
hilo lilifunguliwa rasmi na Mama Salma tarehe 15.10.2013.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wahisani
kutoka nchini Italia wakiongozwa na Balozi wan chi hiyo hapa Tanzania
walioshiriki katika ujenzi wa Jengo la wodi ya watoto mkoani Iringa.
PICHA NA JOHN LUKUWI.
0 comments:
Post a Comment