Na Lorietha Laurence-Maelezo
……………………………………………
NAIBU Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe.Pereira Silima atafungua kikao cha bajeti
ya shirika la Magereza kwa mwaka wa fedha2013/2014 Oktoba 21 mwaka huu
mjini Morogoro.
Kikao
hicho kitashirikisha wajumbe 94 wakiwemo maafisa waandamizi kutoka
makao makuu ya Jeshi la Magereza,Wakuu wa Miradi ya Magereza na
wasimamizi wa miradi hiyo.
Katika
kikao hicho wajumbe watajadili taarifa za utekelezaji wa bajeti
iliyopita ya mwaka wa fedha 2012/2013 kwa kuangalia mafanikio na
changamoto zilizojitokeza kwa kipindi hicho na kuwasilisha bajeti ya
mwaka wa fedha 2013/2014.
Shirikisha
la Magereza linashughulika na miradi mbalimbali ya kiuchumi ambayo ni
kilimo , mifugo , viwanda vya kutengeneza viatu,sabuni,samani za ofisini
na majumbani pamoja na uzalishaji wa chumvi.
Kikao hicho kitarajiwa kufungwa Oktoba 22 mwaka huu na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Bw.John Minja.
0 comments:
Post a Comment