Friday, October 4, 2013


1239581_432061306914560_864943343_nNa Baraka Mpenja wa Fullshangwe, Mbeya
Wakati wapenzi wa soka jijini Mbeya wakisubiri kwa hamu kuona nini klabu yao ya Mbeya City itavuna kesho katika uwanja wa Sh. Amri Abeid jijini Arusha dhidi ya JKT Oljoro katika mchezo wa ligi kuu soka Tanzania bara, benchi la ufundi la klabu hiyo limetamba kufuta matokeo ya sare za mfululizo tangu kuanza kushiriki ligi.
Akizungumza na mtandao wa FULLSHANGWE kwa njia ya simu kutoka Arusha, kocha msaidizi wa klabu hiyo, Maka Mwalwisyi amesema wamefanya mazoezi mazuri , huku vijana wao wakiwa na morali ya kupambana na maafande wa Oljoro ili kujipatia pointi tatu muhimu.
“Tunamshukuru Mungu vijana wapo salama, tumefanya mazoezi hapa Arusha na kizuri hali ya hewa ya hapa haina tofauti na Mbeya, hivyo haitaweza kuathiri mchezo kwa namna yoyote ile”. Alisema Maka.
Maka alisisitiza kuwa benchi la ufundi chini ya Kocha mkuu, Juma Mwambusi limechoshwa na sare nyingi za mfululizo, hivyo katika mchezo wa kesho watapambana kufa na kupona kuhakikisha wanaibuka na ushindi na kuendelea kujenga imani kubwa kwa mashabiki wao.
“Niwaombe mashabiki wa Mbeya kuwa na imani na timu yao, watuombee dua njema kwa mwenyezi Mun gu ili mipango yetu iende sawa. Kama ni maandalizi, kwa asilimia kubwa tumefanya na tunasubiri m uda wa mechi ufike tukafanye yetu uwanjani”. Alisema Maka.
Pia kocha huyo ambaye ni muumini mkubwa wa soka la Vijana aliongeza kuwa kwa sasa timu yao imekuwa gumzo kubwa nchini Tanzania kutokana na kiwango chake, hivyo wanapata changamoto kubwa ya ushindani kutoka kwa timu pinzani.
Mbeya City wataingia uwanjani wakiwa na kumbukumbu ya kutoka sare ya bao 1-1 mechi iliyopita dhidi ya Coastal Union katika Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Kwasasa City wapo nafasi ya 8 katika msimamo wa ligi kuu soka Tanzania bara wakijikusanyia pointi 8 kibindoni.
Klabu hii yenye mvuto mkubwa kwa sasa ilianza ligi kwa kutoka sare na Kagera Sugar, ilishinda mabao 2-1 dhidi ya Ruvu Shooting,  ikatoka sare ya 1-1 na Yanga, pia wakatoka sare ya 1-1 na Coastal, mechi zote zilichezwa Sokoine.
Mechi ya kwanza kucheza ugenini ilikuwa dhidi ya Mtibwa Sugar Uwanja wa Manungu Complex na baadaye ikasafiri mpaka Dar es salaam kukabiliana na Simba na kutoa sare ya mabao 2-2, Uwanja wa Taifa.
Na hapo kesho inacheza mechi ya tatu ugenini ambayo ni mechi ya saba mpaka sasa dhidi ya JKT Oljoro jijini Arusha.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video