MASHABIKI
wa Arsenal wamejawa hofu baada ya kuona picha za kiungo Jack Wilshere
akiwa ameinua mguu wake akipozwa maumivu kwa barafu baada ya kutolewa
nje na kukaa benchi.
Wilshere
alianza kwenye kikosi cha The Gunners kilichomenyana na Borussia
Dortmund katika Ligi ya Mabingwa Ulaya dakika ya 58 wakati huo timu hizo
zikiwa zimefunana bao 1-1.
Santi
Cazorla akaingia kuchukua nafasi ya Wilshere Uwanja wa Emirates na
mwishowe Arsenal ikalala 2-1 mbele ya wababe hao wa Ujerumani.
Kiungo
huyo England mwenye umri wa miaka 21, alijigonga nyuma ya lango la
Roman Weidenfeller katika harakati za kugombea mpira kipindi cha kwanza.
Alimalizia daika chache za kipindi cha kwanza kabla ya kocha Arsene Wenger kumtoa mapema kipindi cha pili.
Ameumia: Wilshere akiwa ameshika kifundo cha mguu wake wa kulia nyuma la lango katika mchezo huo
Maumivu: Wilshere alionekana hayuko vizuri baada ya kulala chini
Wilshere alipigwa picha akiwa amekaa sambamba na wachezaji wengine wa
akiba amevaa jaketi la Arsenal na mguu wake umefunikwa kwa barafu.
Licha ya mabadiliko hayo, Wilshere anaamini atakuwa fiti kwa mchezo wa
Ligi Kuu ya England dhidi ya Crystal Palace mwishoni mwa wiki.
Kazini: Wilshere akipambana katika safu ya kiungo jana ya Arsenal jana
Katika mchezo huo, Henrikh Mkhitaryan aliwafungia wageni bao la
kuongoza kabla ya mshambuliaji pekee wa Arsenal, Olivier Giroud
kukisawazisha kikosi cha Wenger.
Lakini Robert Lewandowski, mfungaji bora wa Dortmund, akawamaliza Arsenal nyumbani kwa bao la dakika za lala salama.
0 comments:
Post a Comment