Wednesday, October 23, 2013

Waziri Mhandisi Christopher Chiza akifafanua jambo Waziri Chiza akiwa na Balozi Kallaghe mkutanoni 
Waziri Chiza akiwa na Balozi Kallaghe mkutanoni Mheshimiwa Waziri Chiza akihutubia kikao cha Reform Club 
Mheshimiwa Waziri Mhandisi Chiza akihutubia kikao cha Reform Mbunge Henry Bellingham katikati akiwa na mfanyabiashara Byran Shand -kulia na mwenzake 
Mbunge Henry Bellingham katikati akiwa na mfanyabiashara Byran Shand -kulia na mwenzake
……………………………………………………………………………………
Imeandaliwa kwa ushirikiano wa Urban Pulse na Freddy Macha 
Wawekezaji wamehimizwa kutosikiliza propaganda za uongo kuhusu uporaji ardhi Tanzania na kuendeleza miradi  ya kilimo nchini.
Akiongea katika  mkutano wa wafanyabiashara na viongozi wa taasisi, mashirika na makampuni  mbalimbali ya ukulima na mazao Uingereza na Tanzania, Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika,  Mhandisi Christopher Chiza alisisitiza serikali iko tayari kumsaidia yeyote anayetaka kuchangia idara hii muhimu ya uchumi.
Waziri Chiza  aliyewasili London Jumatatu,  kwa ziara ya kiserikali ya siku tano akiongoza msafara wa wanataaluma  wa kilimo, alikuwa akijibu swali lililoulizwa mara kadhaa kuhusu ugawaji ardhi Tanzania.
Alifafanua: “ Lipo gazeti moja lilisema serikali imechukua hekta milioni tatu. Si kweli. Ardhi  iliyoshakaguliwa katika miaka miwili iliyopita si zaidi ya hekta 4,000. Habari hizi zimesababisha Tanzania kuondolewa katika kundi la nchi za kuwekeza kilimo.  Hata wafanyakazi wa mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) yanatangaza uongo huu ambao ni marudio tu ya mambo yasiyo kweli yaliyoshazushwa zamani. Tafadhali njooni muongee na sisi wizarani na serikalini  au taasisi zinazoaminika kama SAGCOT. Tutawaambia ukweli na kufanya nanyi kazi.”
Mkutano husika ulifanyika ukumbi wa Reform Club mtaa wa Pall Mall, London, na kuhusisha  wafanyabiashara wenye shughuli za kilimo Tanzania, makampuni makubwa yanayojishughulisha  bara Asia, Afrika na Uingereza, mathalan duka maarufu la Sainsburys.
Kati ya wazungumzaji wakuu alikuwa Balozi  wetu, Uingereza, Mhe Peter Kallaghe aliyesisitiza sera ya Tanzania kuendeleza mahusiano ya kibiashara badala ya kutegemea sana misaada ya kigeni; Rachel Turner  mkurugenzi wa tawi la Mashariki na Afrika ya kati, idara ya serikali ya Uingereza ya Maendeleo ya Kimataifa (DFID);   Afisa Mtendaji Mkuu wa kituo cha mpango maalum wa uendelezaji kilimo ukanda wa Kusini Tanzania ( SAGCOT), Geoffrey Kirenga na Profesa Peter Mahamudu Msolla,  Mwenyekiti wa Kamati ya Wabunge  ya Kilimo, Mifugo na Maji.
Katika hotuba yake Waziri Chiza alifafanua malengo matatu muhimu kuhusu ziara hii, yaani kuendeleza fursa ya kibiashara na uwezekaji, kujifunza teknolojia zinazohitajika na kuwaeleza wakulima na wafanyabiashara mambo takikana.
Msisitizo wa uwekezaji kupitia sekta binafsi ulitolewa mfano mzuri na Bwana Carter Coleman, Afisa Mtendaji wa  Agrica linaloongoza mradi wa kuendeleza hifadhi, misitu na kilimo bora Afrika Mashariki.
Coleman ambaye amekuwa na mahusiano ya karibu na Tanzania toka 1987 alieleza baadhi ya shida zinazokabili kilimo kwa kusisitiza kuwa “ kilimo Afrika ni aghali kuliko sehemu nyingine zote duniani.”
Alitaja baadhi ya matatizo makuu kuwa kupatikana kwa umeme, ghala na hifadhi za mazao, matengenezo ya vifaa kama trekta, maradhi ya mimea na kujua mbegu zipi zitumike wapi na vipi.
“Kutokana na hayo kitengo cha uwekezaji na biashara ya binafsi ni muhimu sana kuendeleza kilimo Afrika,” alikumbusha. 
Mheshimiwa Waziri Chiza anatazamiwa kukutana na Watanzania leo Jumatano katika ukumbi wa Ubalozi wa Tanzania London, uliomtayarishaji mkuu wa safari hii nzima.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video