Friday, October 4, 2013


Prime-Minister-Mizengo-Pinda5
Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
 WAKAZI wa kijiji cha Twabagondozi wilayani Kibondo, Kigoma wamemuomba Waziri Mkuu Mizengo Pinda awasadie kuharakisha upatikanaji wa zaidi ya sh. milioni 660 ili waweze kukamilisha uchimbaji wa mfereji mkuu wa mita 2,500 katika mwaka 2013/2014.
 
Wametoa ombi hilo jana mchana (Alhamisi, Oktoba 3, 2013) wakati wakiwasilisha taarifa ya mradi wa ujenzi wa bwawa la umwagiliaji la Nyendara lililopo katika kijiji cha Twabagondozi wakati Waziri Mkuu alipotembelea mradi huo kuona maendeleo yake.
 
“Ili kukamilisha uchimbaji wa mfereji, katika mwaka 2013/2014, Halmashauri imeomba kiasi cha sh. 660,627,000 kutoka mfuko wa Mfuko wa Umwagiliaji wa Wilaya (DIDF) ili kuchimba mfereji mkuu wa mita 2,500, kujengea mfereji huo, kujengea vigawa maji vinne, kujenga eneo la kunyweshea mifugo,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo.
 
Akisoma taarifa hiyo mbele ya Waziri Mkuu, Katibu wa Mradi wa Bwawa la Nyendara, Bw. Alphonce Chimelese alisema wanahitaji pia kujenga daraja la kuvuka mfereji mkuu kwenda kijiji cha jirani cha Bitare. “Tunaomba utilie mkazo upatikanaji wa fedha hizi ili tukamilshe ujenzi wa mradi wetu,” aliongeza.
 
Ujenzi wa bwawa hilo ulioanza Novemba, 2011 na kukamilika Januari, 2013 umegharimu sh. milioni 640 ambazo ni ruzuku kutoka Serikali Kuu kupitia Mfuko wa Umwagiliaji ngazi ya Wilaya (District Irrigation Development Fund-DIDF).
 
Bwawa hilo lina ukubwa wa kilometa za mraba 9.8 na wastani wa kina cha mita 10.8 ambapo ujazo wake ni lita milioni 758.7.
 
Bw. Chimelese alisema kukamilika wa mradi huo, kutaongeza tija yauzalishaji wa zao la mpunga kutoka tani 2.9 kwa hekta za sasa na kufikia tani 5.2 kwa hekta ifikapo mwaka 2015/2016.
 
“Vilevile, mradi utanufaisha kijiji kwa kuongeza eneo la kilimo cha umwagiliaji hadi kufikia hekta 400 za mpunga wakati wa kiangazi ikilinganishwa na hekta 160 zinazotumika hivi sasa,” alisema.
 
Waziri Mkuu ambaye alikuwa katika siku ya tatu ya ziara yake mkoani Kigoma aliwapongeza wakazi wa kijiji hicho kwa kuibua mradi huo kupitia kwenye Halmashauri yao. Aliwahimiza wapande vifaranga vya samaki kwenye bwawa hilo ili waweze kuongeza shughuli za uchumi katika wilaya yao na kujiongezea kipato.
 
Katika ziara hiyo ya siku sita mkoani Kigoma, Waziri Mkuu amefuatana na mkewe Mama Tunu Pinda, Waziri wa Nchi (OWM-TAMISEMI), Bibi Hawa Ghasia, Naibu Waziri wa Maji, Dk. Binilith Mahenge, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Bw. Lazaro Nyalandu pamoja na Naibu Waziri Nishati na Madini, Bw. George Simbachawene.
 
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
IJUMAA, OKTOBA 4, 2013.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video